THREE THOUGHT THAT CAN CHANGE YOUR LIFE. (Mawazo matatu yanayoweza kubadili maisha yako)

Maisha,  ni kitu cha kushangaza sana. Laiti yangekua na fomula basi na uhakika kila mmoja agejifunza hiyo fomula ya maisha. Kwa maana naamini kua kila mmoja haijalishi anaishi maisha ya aina gani,  baai mtu huyo anataka kuyabadili maisha yake. Kama ni tajiri basi atataka kua tajiri zaidi. Na kama masikini basi utajiri ndio kitu unachokitafuta kwa nguvu zote. Labda huitaji utajiri ila umelidhika tu na maisha yako ya kila siku. Lakini kimoja ambacho ninachofahamu kwa uhakika ni kua kila mtu anataka kubadili nyanja fulani ya maisha yake. Kama sio maisha yake yote basi nyanja fulani ya maisha yako baai unataka yabadilike.

Iwe unataka kubadili maisha yako yote na kua tajiri au unataka kubadili nyanja fulani ya maisha yako basi mawazo haya matatu yanaweza kubadili maisha yako kabisa kama ukitatilia maanani na kuyafuata kwa usahihi.

WAZO LA KWANZA

ISHI KWA KUMTEGEMEA MUNGU
Katika maisha haya ni vigumu sana kuishi maisha ya kumtegemea mtu au kutegemea akili zako. Kwa maana wengi sana wamejaribu na wengi sana wameshindwa. Kwa maana ukimtegemea binadamu atakunyanyasa na atataka uishi maisha yako vile anavyotaka yeye. Na ukitegemea akili zako bado huwezi kufanya lolote kwa huwezi hata kuongeza urefu wa unywele wako kwa kujihangaisha.Sasa utaona kua kumtegemea binadamu au kiumbe chichote ni sawa na kujirisha upepo na ni ubatili mtupu.

Biblia inasema kua amtegemeaye mwanadamu amelaani lakini yule ambaye anamtegemea mungu amebarikiwa na anakha kama mti uliopandwa kandokando ya chemchem kamwe hautaona kiu wala njaa wakati wa kiangazi. Mungu ndie baba yetu alietuumba hivyo anajua jana yetu,  leo yetu na keaho yetu. Hivyo ni jambo la busara kumtegemea yeye.

Nakumbuka wakati fulani mtu aliwahi kuniambia kua kiumbe chochote chenye busara kinachoishi katika ulimwengu wenye vurumai na vurugu na chenyewe ni dhaifu basi hutafuta kiumbe kingine chenye nguvu zaidi yake ili kiungane nae.

Em niambie utajisikiaje pale utakapo kua unamtegemea jemedary ambaye hajawahi kushindwa vita? Mmh itakua vizuri sana si ndio?
Basi mtegemee mungu ili ubadili maisha yako.

WAZO LA PILI
UPENDO
Katika ulimwengu wa sasa ambao umejawa na dhuruma na uovu wa kila aina,  upendo ni bidhaa hadimu sana. Katika ulimwengu uliotawaliwa na chuki,  hasira,  kisasi na kila aina ya uaini upendo ndio dawa pekee ambayo inaweza kutibu kila majeraha na kufuta kabisa kila kovu.

Kuna mtu aliwahi kusema kua "hasira, chuki na kisasi hivi ni vitu vinavyotumiwa na adui ili kutugawanya. Kama tukiweza kuvishinda hivi vyote basi tutagundua kua sisi ni zao la upendo na sio chuki,  furaha na sio hasira hivyo upendo ni silaha,  ngao na ni dawa 

WAZO LA TATU
USIKATE TAMAA
Katika maisha hakuna kitu kinachokuja rahisi rahisi tu. Hivyo kunahitajika jitihada na kua king'ang'anizi bila kukata tamaa au kusikiliza watu wanasemaje kwa maana binadamu kajawa na husda hataki kumuona mwenzake kafanikiwa hivyo hawatakwisha kukukatisha tamaa. Basi jifunze kua kukata tamaa ni mwiko na jua ya kwamba hakuna kitu ambacho kitakaa milele au hali ambayo haitabadilika kwa maana kila kitu ni lazima kibadilike hivyo ndivyo mzunguko wa maisha ulivyo.

Lakini  ni lazima tujue ya kua mabadiliko katika maisha yetu yanategemea sana mawazo yetu. Mawazo ndio hatua ya kwanza kabisa ili kuleta hayo mabadiliko unayoyataka hivyo kama ukijifunza kuwaza mawazo mema na sio mawazo mabaya sio tu utabadili maisha yako ila utakua master wa maisha yako mwenyewe.

Mwanafilosofia mmoja waliwahi kusema " not just thought but the application of right thoudht its a conner stone of every change in ones life"Published from Blogger Prime Android App
THREE THOUGHT THAT CAN CHANGE YOUR LIFE. (Mawazo matatu yanayoweza kubadili maisha yako) THREE THOUGHT THAT CAN CHANGE YOUR LIFE. (Mawazo matatu yanayoweza kubadili maisha yako) Reviewed by Maktaba on October 12, 2021 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.