Give and Take

 KITABU : GIVE AND TAKE
MWANDISHI : ADAM GRANT
MCHAMBUZI : QUNCE MARK JOHN

UTANGULIZI.

Give and take in kitabu kinachozungumzia sana tabia za watu pale tunapokutana na watu wengine. iwe ni nyumbani, kazini, au mazingira yoyote Yale binadam huwa anakua na tabia tatu ambazo ni
GIVERS, TAKERS na MATCHERS.

GIVERS

Givers ni watu ambao wanapenda kutoa au kujitoa kwa ajir ya watu wengine. na wapo tayari hata kurisk maisha yao au walichonacho kwa ajir ya mtu mwingine. bila kuhitaji wala kufikiria kitu chochote kama malipo.

TAKERS
takers hawa ni watu tofauti kidogo wenyew wanapenda kupata wapo tayari kupata kitu wanachokitaka hata kama ni kwa kurisk au kutoa maisha ya watu wengine. takers hawafikirii hitaji la mtu mwingine isipo kua lao. na wapo tayari kulipata kwa gharama yoyote ile hate kama ni kwa gharama ya mtu mwingne.

MATCHES

Matchers ni watu wanaopenda nipe nikupe. hawa watu ikitokea ukawaomba msaada watakuuliza ni kitu gani watapata baada ya msaada watakao kupa. matchers wanapenda wakikupa kitu na wao wapate.

kadri tunavyoendelea kukichambua kitabu hiki kizuri ndivyo tutakavyoona kiundani zaidi hizi tabia tatu zinavyopelekea mafanikio ama kushindwa katika maisha yetu ya kila siku

CHAPTER 1

 GOOD RETURNS
 Hasara na Faida ya Kutoa sana kuliko unavyopata
Mwandishi anaanza na story ya watu wawili Danny na David. Danny akiwa ni mjasiriamali was mtandaoni ambae akiwa na miaka 30 alianzisha kampuni yake ya kwanza. na tayri sas hiv anatengeneza kampuni yake ya nne.
David yeye ni mwekezaji ambae husikiliza mawazo ya wajasiriamali na kuamua kuyapa mitaji au laah.

Baada ya David kusikiliza wazo la Danny. haraka sana alijua kua wazo lake ni zuri sana na kama wawekezaji wengine wangelisikia wange panga foleni kutaka kuingia mkataba na Danny.

David akafanya kama ambavyo mwekezaji yoyote anaweza kufanya akampa Danny terms za makubaliano kama akikubali basi wasaini mkataba na David alijua kua kama akifanya haraka basi anaweza kusaini mkataba na Danny na akafanya nae kazi badala yake David akamwambia Danny kua anaweza akachukua mda kufikiria zaidi juu ya makubaliano aliyoyatoa na kama akiweza akutane na wawekezaji wengine ili aweze kulinganisha offer yake na yao. baadae David akamtumia Danny list ya references ambao wangeweza kutoa ushuhuda juu ya uwezo wa David katika kufanya kazi.

Danny akafanya kama alivyoshauliwa na David akatumia wiki moja kukutana na wawekezaji wengine na kuwambia juu ya wazo lake. mwisho wa siku Danny akampigia simu David akimwambia kua anasaini mkataba na wawekezaji wengine.
mwandishi anasema financial terms alizotoa David na wawekezaji wengine zilikua ni sawa.


Danny alijua kua David mtu mzuri ambae kama angefanya nae kazi basi angekua ana mtia moyo badala ya kumchallenge. wawekezaji wengine wanafahamika kwa kumsukuma na kumchallenge mjasiriamali kufikia malengo kitu ambacho Danny alihisi kua David hana. mwandishi anasema kilichomponza David ni kua mtu mwema na kufikiria maslahi ya mtu mwingine zaidi ya kwake.

 Mwandishi anasema kua vitu ambacho watu wenye mafanikio wanavyo vinafanana ni MOTIVATION (motisha), ability (uwezo) na opportunity (nafasi). lakini kama tunataka mafanikio tunahitaji mchanganyiko wa KUFANYA KAZI KWA JUHUDI, TALANTA na BAHATI lakini pia tunahitaji kitu kimoja ambacho ni muhimu sana ambacho ni jinsi gani tunaingiliana na watu wengine au jinsi gani tunatengeneza mahusiano na watu wengine.

 kila mda tunapoingiliana na watu wengine iwe ni kazini ama sehemu yoyote ile lazima tujiulize je tunataka kuongeza uthamani wetu binafsi au tunataka kuongeza uthamani wa watu wengine bila kujali ni kitu gani tunapata.

TAKERS wako toufauti kidogo wanapenda kupata sana kuliko wanavyotoa. wanapenda kuweka mahitaji yao mbele kuliko ya watu wengine, takers wana amini kua dunian hapa ni sehem ya mashindano, dog-eat-dog place.
wanahisi kwamba ili kufanikiwa wanahitaji kua bora kuliko wengine na kufanya vizuri kuliko wengine.
takers sio wakatili au wanaroho mbaya ila wanapenda kua makini na pia kujilinda kwa kila kitu wanachokifanya.
takers anajua kua kama nisipojilinda mwenyew basi hakuna atakae nilinda.

kama David angekua takers angehakikisha anampa Danny deadline na kuhakikisha kua anaingia mkataba na Danny. lakini David sio takers ni Givers,wanaopenda kujitoa kwa watu wengine na kutoa zaidi kuliko wanavyopata, givers wako focused sana na kitu gani watu/MTU anahitaji kutoka kwake.

Givers and takers wanatofautiana kwenye tabia na matendo yao kwa watu wengine, kama wew ni taker unawasaidia watu pale tu unapoona unapata faida na faida iwe kubwa kuliko unachokitoa.
na Givers wenyew wanawasaidia watu bila kuhitaji malipo au kupata kitu chochote kama mrejesho wa msaada alioutoa.

CHAPTER 1

 GOOD RETURNS PART 2

 _Hasara na Faida ya Kutoa sana Kuliko Unavyopata 
_
mwandishi anasema kua kuna utafiti ulifanyika ili kujua kua ni group lipi Kati ya takers, givers and matchers lina mafanikio makubwa kimaisha na lipi lina mafanikio madogo kuliko mengine yote.

utafiti huu ulihusisha  mainjinia, wanafunzi wa udaktari na watu wa mauzo. utafiti ulionyesha kua katika magroup yote, group ambalo lina mafanikio kidogo kuliko yote ni GIVERS kwa sabab givers wanatumia mda mwingi sana kusaidia watu wengine zaida ya kufanya shughuli zao binafsi ambazo zinaweza kuwapatia maendeleo binafsi.

kwa kua GIVERS ni watu wenye mafanikio madogo kuliko magroup mengine he unaweza kuhisi ni group lipi kati ya TAKERS na MATCHERS wenye mafanikio makubwa??

mwandishi anasema baada ya kuziangalia data vizur na kuzifanyia utafiti tena aligundua kua sio TAKERS wala MATCHERS ambao wana mafanikio makubwa ila ni GIVERS tena kwa sabab japo kua givers wanaonekana kama ni losers kwa upande mmoja kwa upande mwingine ni winner kwa maana kitendo chao cha kuacha kazi zao na kusaidia watu wengine kinawajengea uaminifu kwa watu in a long run kitu ambacho kinawaletea mafanikio baadae.

Story ya David na Danny haikuiishia pale kwa sababu baada ya Danny kusaini mkataba na mwekezaji mwingine alihisi kutokua na furaha juu ya kitendo alichomfanyia David kwa hyo kabla kampuni yake haijafunga nafasi za kutafuta wawekezaji Danny akataka amlete David lakini njia pekee ya kumleta sio kama mwekezaji tena ila kama mmiliki wa kampuni kitu ambacho Danny akaona kua its worth the risk  kuliko kuishi na guilty ya kitendo alicho kifanya.

kwahyo at the end David anafanya kazi na Danny sio kama mwekezaji tena ila kama co-owner wa kampuni.



CHAPTER 2

 THE PEACOCK AND THE PANDA 
 Jinsi Gani Givers, Takers na Matchers wanatengeneza Network

kwa karne sasa tunatambua unuhimu we kutengeneza mtandao (networking). na mtandao huu unakua na faida tatu kubwa ambazo ni KUPATA TAARIFA, KUPATA STADI TOFAUTI TOFAUTI na NGUVU. kwa kutengeneza mtandao imara mtu anaweza kupata MAARIFA, UTAALAMU na USHAWISHI.

utafiti unaonyesha kua watu wenye mitandao imara wanakua na utendaji mkubwa,wanapata pesa nyingi na pia get promoted faster.

kwa takers kutengeneza mtandao ni njia ya wao kujipatia wanachokita na Mara nyingi taker huwa anabadili tabia na kujifanya kua matcher ili tu kufit kwenye mtandao anaoutengeneza. kwa kifupi takers wanakua fakers

katika upande mwingine GIVERS and MATCHERS wanaona kua kutengeneza mtandao kama njia ya kuconnect na watu wapya na mawazo mapya.

mwandishi anasema katika chapter hii atazungumzia zaidi jinsi ambavyo takers, givers na matchers wanatengeneza mtandao yao na jinsi ambavyo tabia zao zina athiri mahusiano yao katika mitandao hiyo.

 _Jinsi ya Kumtambua Taker Anaejifanya Kua Giver_
Ili Taker aweze kuingia kwenye mtandao wowote lazima ajifanye kua giver au matcher kwa maana hakuna mtu ambae atakubali kua na ukaribu na mtu ambae anamtumia na mwinsho wa siku ambwage. kwahyo ili taker aifiche ngozi yake halisi hujifanya kua mkalimu na mtoaji kuliko kawaida ( hapa ndo unakuta watu wanaanzisha charity foundation kwa ajir ya kusaidia watu kumbe ni disguise tu) ili waweze kuaminiwa na kukubalika na watu. na kama utataka taker ambae ni faker audhurie kwenye sherehe yako basi alika mtu maarufu hapo atakuja kwa maana takers pamoja na umafia wao wanapenda kuonekana na watu muhimu/maarufu katika jamii.

wadachi wanamsemo kwa watu wenye tabia kama hizi " Kissing up, Kicking down" takers akiwa katika sherehe au mikutano tofauti anapenda " kukiss up" *au kujipendekeza kwa Watu wenye power huku " *akikick down"* watu ambao ni wadogo na wasio kua na faida kwake. kuna msemo moja unasema " _kipimo halisi cha mwanaume ni jinsi gani anamtreat mtu asiekua na umuhimu kwake hata kidogo
Taker may rise by kissing up but they often fall by kicking down

CHAPTER 3

 THE RIPPLE EFFECT 

 Geniuses and Genius Makers

Labda unaweza kumfahamu George Meyer. kama humfahamu basi na uhakika kua utakua unafahamu baadhi ya kazi zake. ni director na script writer maarufu sana katika ulimwengu wa vikatuni moja ya kazi zake ambazo zimeweza kupata tuzo kubwa dunian ni Tv-series ya The Simpson.

watu wake wakaribu wanasema ukikutana nae huyu jamaa ni mtu mcheshi na mtanashati sana ambae anapenda kusaidia watu. na kwa watu anaofanya nao kazi wakiwa wanamzungumzia wanamtaja jamaa kama genius wa kuandika kazi zake.

mwandishi anasema kua wataalamu walifanya utafiti ili kugundua kua kati ya watu wabunifu na wenye akili nyingi na watu wenye akili za kawaida na wenye ubunifu wa kawaida ni kundi lipi ni takers na lipi ni Givers.

Uchunguzi huu uliwahusisha wanasayansi wenye utendaji mkubwa sana katika fani zao na wale wenye utendaji wa kawaida.
utafiti ulionyesha kua wanasayansi wabunifu na wenye utendaji mkubwa kua ni takers kwa sabab kipindi chote cha utafiti walionekana kua ni watu wa kujipendelea wao tu kuliko watu wengine, hawajali hisia za watu wengine na pia walipo kosolewa walishikwa na hasira na kujitetea kwa nguvu zote.

pia walikubaliana na baadhi ya sentence kua mda mwingine wanapata credit kwa kazi ambazo sio zao.

kwa wanasayansi wenye ubunifu wa kawaida hali ilikua tofauti kidogo. walikua supportive kipindi chote cha utafiti na walionyesha tabia za kujali, kutegemewa, na kuweza kuwahurumia watu wengine kitu ambacho kwa watu wenye akili nyingi ama geniuses hawana.

mwandishi anasema Geniuses hawajihisi kama wamefungwa na minyororo ya jamii kwa maana ya kufanya kama ambavyo jamii inataka.

kueleza hili vizur mwandinshi anatumia baadhi ya maneno ya George Meyer ambae kuna wakati alisema " mungu ni mchawi alietengenezwa na watu waoga walioishi mapangoni miaka mingi iliopita"

 CHAPTER 4

 FINDING THE DIAMOND IN THE ROUGH 
 The Fact and Fiction of Recognizing Potential

Obama kipindi anaingia white house aliulizwa na mwandishi was habari kama ana app yoyote anayoipenda, bila kusita Obama akajibu kua anapenda iReggie, ambayo ina vitabu ninavyopenda, miziki na Magazet vyote katika sehemu moja.

The iReggie haikua app kama Obama alivyosema Bali ni mtu ambae jina lake kamili aliitwa Reggie Love, na hakuna aliewahi kuhisi kama angekua mtu wa karibu wa Obama

Reggie Love baada ya kumaliza masomo yake katika chuo cha Duke alipata kazi katika offisi ya Obama katika kitengo cha masijala akiwa kama mtu wa mail, kipindi hicho Obama alikua senetor.
lakini baada ya mwaka mmoja tu Reggie alikua promoted mpaka kufikia kua msaidizi binafsi wa obama.

Reggie alikua anafanya kazi masaa 18 kwa siku na amesafir na Obama zaid ya maili 880000.
uwezo wake wa kukimbizana na majukumu mengi huku akiwa na wakati mdogo wa kulala ulikua ni wakishupavu, alisema Obama.

Miongo michache nyuma katika mji aliotokea Reggie love kulikua na mwanamke ambae alimua kurud shule kusomea uhasibu. ingawa uwezo wake katika hesabu haukua mzur. mwanamke huyu alijulika kwa jina la Beth Traynham.

Beth ambae mpaka hivi ukubwani alikua anasumbuliwa hesabu za asilimia na alitumia wiki moja kuelewa pansion accounting na mwisho wa siku akajikuta ameelewa kidogo kuliko alivyokua anajua mwanzoni.

ulipofika wakati wa kufanya mtihani wa CPA, Beth alipatwa na panic attack baada tu ya kuyaona maswali ya kuchagua.

Baada ya mtihani kuisha Beth aliondoka akijua kua kafeli mtihani. baada ya wiki moja beth alipigiwa simu na kuambiwa kua amefaulu mtihan, baada ya kusikia hiz taarifa beth alijua kua ni utani hivyo akapiga tena simu kutaka kuhakikisha majibu yalikua ni Yale Yale. Leo hii beth ni moja ya wahasibu wanaoheshimika sana.

Reggie Love na Beth Traynham no watu walioishi maisha tofauti lakini wote wanakitu kimoja kinachofanana, walifundishwa na professor C.J. SKENDER a living breathing legend.

SKENDER ni professor wa accounting katika chuo cha Duke na wote love na beth wamefundishwa na huyu jamaa
ustadi wa skender kutambua uwezo was mtu binafsi na kukitengeneza kipaji chake ujuzi unaohitajika karibu katika kila tasnia.

Sio ngumu kusema kwamba tumezungukwa na watu ambao ni nyota na wanauwezo wa hali ya juu kwenye mambo flani flani.

na njia pekee ya kuweza kuvitambua vipaji hivi ni kutumia reciprocity kama njia pekee ya kutambua uwezo walionao watu wengine.


CHAPTER 5

 THE POWER OF POWERLESS COMMUNICATION 

 How to Be Modest and Influence People

Katika hii chapter tutaangali ni jinsi gani givers na takers wanatumia njia gani katika kushawishi watu na ipi ni njia effective in a long run. Kwa sababu mafanikio yanategea sana uwezo wako wa kushawishi.

kushawishi watu wengine kununua bithaa zetu, kutumia huduma zetu, kukubali mawazo yetu na kuwekeza kwetu.

Watafiti wanasema kua kuna njia kuu mbili za kuweza kushawishi watu. njia ya kwanza ni DOMINANCE (kutawala) na PRESTIGE (ufahari)

Pale tunapoonyesha utawala tunapata ushawishi kwa sabab watu wengine wanatuona kua tuna nguvu na wenye mamlaka. na pale tunapopata ufahari tunakua na ushawishi kwa sababu watu wengine wanatuheshimu na kutaman kua kama sisi.

Takers wanavutiwa na kupata utawala, katika jitihada za kupata uthamani haraka zaidi kadri iwezekanavyo. takers wanapenda kuonekana kua wana nguvu juu ya wengine hivyo wanapenda mawasiliano yenye nguvu. wanaongea kwa nguvu nyingi na kupandisha sauti zao kuonyesha mamlaka walionayo, kua imara ili kuoyesha kujiamini, huonyesha mafanikio yao ili waweze kuuza kwa sifa na mda mwingine hutumia vitisho pale vinapohitajika.

katika kupata ushawishi takers wanakua wanatawala mazungumzo kwa kuonesha viashiria vinavyoonekana na visivyoonekana na ndio maana takers wanapata sana utawala kuliko Givers.

Utawala ni zero-sum game: kadri ambavyo wasikilizaji/watu unaotaka kuwashawishi walivyo na nguvu na mamlaka kukushinda ndivyo unavyopoteza ushawishi.

Taker akikutana na mtu mwenye mamlaka na nguvu kushinda yeye ndivyo alivyo kwenye hatari ya kupoteza ushawishi wake.

Kinyume cha mawasiliano yenye nguvu ni mawasiliano yasiokua na nguvu.
mawasiliano yasiokua na nguvu ni pale mtu anaongea bila kutumia nguvu huku akionyesha wasiwasi na akitegemea ushauri kutoka kwa watu wengine. unaongea katika njia inayoonesha udhaifu huku ukionyesha madhaifu.

takers wanaogopa kutumia hii njia kwa sabab kuonyesha madhaifu yao kutaharibu utawala na mamlaka yao.

Givers wanajisikia huru kuonyesha madhaifu yao kwa sabab lengo lao sio kupata mamlaka au ushawishi Bali ni kusaidia watu na sio kuwatawala.


CHAPTER 6

 THE ART OF MOTIVATION MAINTENANCE 

 Kwanini Baadhi ya Givers Wanamafanikio na Wengine Hawana

Mpaka sasa tumekua tukiangalia ni kwa jinsi gani Givers wanapata mafanikio kupitia njia zao za kipekee kama kutengeneza mitandao, ushirikiano, mawasiliano, ushawishi na jinsi gani wana wasaidia watu wengine kufikia mafanikio yao.

kama ambavyo tumeangalia kwenye chapter zilizopita. tumeona givers pia ni watu wa chini kabisa kwenye ngazi za mafanikio.

mafanikio haya angalii tu katika nguvu ya utoaji ila pia ni jinsi gani mtu unaweza ukaepuka anguko LA kijinga.

kama ukiwa mtoaji sana utaishia kujitoa sadaka kwa mafanikio ya watu wengine na kushindwa kufikia malengo yako. na hii hali ya kutoa sana kunapelekea givers wanakosa nguvu na kuchoka pia.

ikiwa njia zinazowafanya baadhi ya givers wanamafanikio na wengine hawana ni vizuri kujua ni kitu gani kina watofautisha  givers wenye mafanikio na wasio na mafanikio.

mwandishi anasema kua kuna givers was aina mbili.
SELFLESS GIVERS na SELF-INTEREST GIVERS.

SELFLESS A GIVER ndo wale wanaojitoa zaidi kuhusu watu wengine kuliko wao binafsi na mda mwingine gharama ya kujitoa kwao inakua kubwa kuliko hats mile walichokitoa

SELF-INTEREST GIVERS ni wale wanaojitoa huku wakiwa na malengo ya kufanya/kupata mambo yao binafsi na pia wanawasaidia watu strategically. kwa mfano unataka msaada kutoka kwake atapanga mda wa kufanya mambo yake na mda was wew kukusaidia.

kama ambavyo Bill Gate alisema kwenye mkutano was dunia kuhusu maswala ya uchumi. alisema " There are two great forces of human nature: self-interest and care for others," and people are more successful when they are driven by a "HYBRID ENGINE" of the two.  kama takers ni. selfish, na giver wasiokua na mafanikio ni selfless basi giver wenye mafanikio wanatabia za aina mbili ni selfless af pia ni self-interest.
Wanawasaidia watu lakini pia wanahakikisha kua mambo yao yanaendelea na yanafanikiwa.
Give and Take Give and Take Reviewed by Maktaba on January 04, 2020 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.