AS A MAN THINKETH

KITABU: AS A MAN   THINKETH
MWANDISHI: JAMES ALLEN
MCHAMBUZI: FRANK LUMATO

UTANGULIZI

AS A MAN THINKETH ni  kitabu kinachohusu matumizi sahihi ya mawazo mwandishi amejaribu kuonyesha madhara ya mawazo kwa binadam mwenyewe kama zikitumika vibaya, mwandishi, ameeleza ni jinsi gani mawazo yanaweza kuathiri mwili wa mwanadamu, jinsi gani mawazo yanaweza kuathiri tabia, jinsi  mawazo yanaweza kuathiri malengo ya mtu,  jinsi mawazo yanaweza kuathiri mazingira na mengine mengi tutakayo yaona ndani ya kitabu chetu kizuri

CHAPTER 1
THOUGHT AND CHARACTER
(MAWAZO NA TABIA)
Mwandishi Anasema Binadamu Anavyojifikiria Moyoni Mwake Ndivyo Alivyo. Sio Jinsi Tu Anavyojikubali Jinsi Alivyo Ila Ni Jinsi Anavyokua Na Uelewa Na Kukabiliana Na Kila Hali Ya Maisha.
Binadam Ni Jinsi Anavyojifikiria Tabia Zake Zinatokana Na Jumla Ya Mawazo Yake Yote, Kama Mmea Jinsi Unavyotokana Na Hauwezi Kua Bila Mbegu Ndivyo Kila Tabia Ya Mwanadamu Inatokana Na Mbegu Iliyojificha Ya Mawazo
Hii Hujumlisha Hata Zile Tabia Zinazotendwa Bila Kufikirika Na Zile Ambazo Hufikiriwa Kabla Ya Kutendwa.

Tabia Ni Kuchanua Kwa Mawazo Na Mateso Na Furaha Ni Matunda Yake Na Ndivyo Binadam Humpata Machungu Na Matamu Huwa Ni Matunda Yake Mweyewe.

Mawazo Katika Akili Zetu Ndizo Zitujengazo Jinsi Tulivyo. Kwa Mawazo Twabomoa Na Kujenga. Hapa Wazungu Huwa Wanakamsemo Wanasema "desire Create, Greed Destroys"
Kama Akili Ya Mwanadamu Ikawaza Mawazo Wabaya Basi Machungu Yatamkuta Na Kama Mtu Akiwazo Mawazo Mazuri Basi Furaha Itamfuata Kama Kivuli Chake

Mwandishi Anasema Tabia Nzuri Na Za Kimungu Sio Kitu Cha Upendeleo Ila Ni Matokeo Asili Ya Muendelezo Na Jitihada Za Fikra Sahihi

Wandish Anasema Binadamu Anajitengeneza Na Kujiharibu Mwenyewe, Katika Mawazo Yake Anatengeneza Silaha Ambazo Zinaweza Kumharibu Mwenyewe Na Pia Katika Mawazo Yake Hayo Hayo Anatengeneza Vifaa Ambavyo Vinamletea Furaha Nguvu Na Amani.

Kwa Chaguo Sahihi Na Matumizi Mazuri Ya Mawazo Yake Binadamu Anakua Kiumbe Kamili Ila Kwa Matumizi Mabaya Ya Mawazo Yake Binadamu Anashuka Na Kua Chini Zaid Ya Mnyama.

Kwa Yote Mazuri Kuhusu Roho Ya Mwanadamu Ambayo Yanafahamika Katika Miaka Hii Hakuna Ambao Umejaa Matumaini Na Ahadi Za Kimungu Kama Hii Kua " Binadamu Anaweza Kuyatawala Mawazo Yake, Mtengenezaji Wa Tabia Zake, Na Mfanyaji Na Mchongaji Wa Mazingira Yake, Hali, Na Matarajio Yake.
Akiwa Kama Kiumbe Mwenye Nguvu, Akili, Upendo, Na Bwana Wa Mawazo Yake, Binadamu Anao Ufunguo Wa Kila Hali Na Anavyo Vitu Ndani Yake Vimsaidiavyo Kuchagua Kua Vile Atakavyo.

Mwandish Anasema Binadamu Siku Zote Ni Bwana, Hata Akiwa Katika Hali Dhaifu Kiasi Ila Katika Udhaifu Wake Ni Bwana Mpumbavu Alieshndwa Kujitawala Yeye Mwenyewe.

Ila Pale Anapoanza Kufikiria Hali Yake Na Kutafuta Kanuni Zinazojenga Mawazo Yake Hapo Anakua Bwana Mwenyewe Busara Alieamua Kutumia Nguvu Zake Na Akili Zake Kutengeneza Upya Mawazo Yake. hapo anakua Bwana Anaejitambua

Na Binadam Anaweza Kua Bwana Anayejitambua Kwa Kugundua Ndani Yake Kanuni Na Sheria Za Mawazo Ambazo Ugunduzi Wake Unatokana Na Kujifanyia Uchunguzi Ndani Yake Kwa Kupitia Tahajudi (meditation)
Mwandishi Anasema Kwa Kutafuta Na Kuchimba Ndipo Dhahabu Na Almasi Hupatikana Ndivyo Binadamu Anavyoweza Kupata Muunganiko Na Mungu Kwa Kuchimba Ndani Kabisa Ya Mgodi Wa Roho Yake Na Hapo Ndio Anakuwa Mtengenezaji Wa Tabia Zake Na Mjengaji Wa Maisha Yake Anaweza Kuhakikisha Hili Kwa Kutawala Na Kubadili Mawazo Yake Na Kuangalia Madhara Juu Yake Na Wengine.

CHAPTER 2
THE EFFECT OF THOUGHT ON CIRCUMSTANCES
(ATHARI YA MAWAZO KATIKA MAZINGIRA)

Mwandishi Anasema Akili Ya Mwanadamu Inaweza Kufananishwa Na Bustani, Ambayo Inaweza Vizuri Au Ikaachwa Na Magugu Yakaota Ila Ilimwe Ama Isilimwe Ni Lazima Itazaa, Kama Kama Mbegu Nzuri Hazikupandwa Basi Magugu Yataota Na Kuendelea Kuzaliana.

Kama Vile Mkulima Wa Bustani Jinsi Anavyoilinda Bustani Yake Isiingiliwe Na Magugu Na Kupanda Maua Na Kila Aina Ya Miti Mizuri Aipendayo, Ndivyo Binadamu Anatakiwa Kuihudumia Bustani Ya Akili Yake, Kutoa Mawazo Yote Mapotovu Na Mabaya Na Kuilima Vizuri Na Kupanda Miti Izaayo Matunda Mazuri

Kwa Kufanya Hivi Binadamu Atagundua Kuwa Ni Bwana Shamba Wa Roho Na Akili Yake, Muongozaji Wa Maisha Yake Na Atagundua Ndani Yake Kanuni Za Mawazo Yake, Na Ataelewa Jinsi Gani Nguvu Ya Mawazo Inavyootengeneza Tabia Yake, Mazingira, Na Matarajio.

Mawazo Na Tabia Ni Kitu Kimoja Ila Tabia Inaonekana Katika  Hali Na Mazingira. Muonekano Wa Nje Wa Binadamu Unategemea Sana Hali Yake Ya Ndani. Hii Haimanishi Kuwa Hali Binadamu Kwa Muda Fulani Ndio Kipimo Cha Tabia Yake Nzima Ila Hali Ile Inakuwa Imeungana Na Baadhi Ya Mawazo Muhimu Ambayo Kwa Mda Huo Ndio Yaliotawala Maendeleo Yake

Mwandishi Anasema Kuwa Roho Inavuta Kila Ambacho Kwa Siri Kimejificha, Kile Ambacho Inakipenda, Na Kile Ambacho Inakiogopa Na Kupitia Mazingira Roho Hupata Kile Inachokivuta

Kila Mbegu Ya Mawazo Iliopandwa Au Akaachwa Ikadondoka Ktk Akili Ya Binadamu Na Ikaota Mizizi, Itazaa Katika Matendo Na Kutoa Matunda Ya Nafasi Na Hali. Mawazo Mazuri Huzaa Matunda Mazuri Mawazo Mabaya Huzaa Matunda Mabaya.
Mazingira Yanachangia Sana Mazingira Ya Ndani Ya Mawazo, Mazingira Mazuri Na Mabaya Ni Vigezo Katika Kumtengeneza Binadamu Mzuri. Kama Mvunaji Wa Mazao Yake Binadamu Anajifunza Kwa Kuumia Na Kufurahi

Mwandishi Anasema Kuwa Kila Binadamu Yupo Pale Alipo Kwa Matakwa Yake Mwenyewe, Kwa Sheria Za Mawazo Alizozijenga Ndani Ya Tabia Zake Zimempeleka Pale Alipo, Na Katika Mipangilio Ya Maisha Hakuna Kitu Kinatokea Tu Ila Yote Ni Matokeo Ya Sheria Ambazo Haziwezi Kukosea.

Kama Kiumbe Anaekua Na Kubadilika, Binadamu Yupo Pale Alipo Ili Ajifunze Kuwa Anaweza Kukua Na Kubadilika. Binadamu Atashindwa Na Mazingira Yake Kama Akiendelea Kuamini Kua Ni Kiumbe Wa Matokeo Ya Nje Ila Kama Akijua Ni Kiumbe Mwenye  Nguvu Ambae Anaweza Kuamuru Mazingira Yake Hapo Anakua Bwana Sahihi

Mwandishi Anasema Sheria Za Mabadiliko Na Ukuaji Zipo Popote Pale, Binadamu Hajikuti Katika Hali Mbaya Eti Kwa Sababu Ya Mazingira Au Matarajio Ila Kwa Njia Za Mawazo Yake Na Tamaa Zake.  Binadamu Mnyoofu Hawezi Tu Kufanya Uhalifu Kwa Kushinikizwa Na Sababu Za Nje Lazima Atakua Na Mawazo Ya Kiaharifu Katika Moyo Wake Na Pale Nafasi Inapojitokeza Basi Hutenda Kile Kilichopo Ndani Yake

Mwandishi Anasema Mazingira Hayamtengenezi Binadamu Ila Yanamuonesha Jinsi Alivyo. Kuna Msemo Wa Kizungu Unasema " The Same Boiling Water That Harden The Egg. Soften The Potatos. So Its Not About Circumstance But What You Made Of"

Mwandishi Anasema Kua Binadamu Ambae Haogopi Kijiumiza Mwenyewe Hawezi Kushindwa Kufikia Malengo Ya Moyo Wake Hata Kwa Yule Binadamu Ambae Anataka Kupata Utajiri Wa Dunia Hii Basi Ajiandae Kujitoa Sadaka Kabla Hajafanikisha Malengo Yake

Namfahamu Jamaa Mmoja Ambae Ni Maskini Na Anataka Sana Kuwa Na Maendeleo Lakini Muda Mwingi Hataki Kufanya Kazi Na Kumdanganya Mwajiri Wake Kuwa Mshahara Anaolipwa Hautoshi. Binadamu Wa Aina Hii Haelewi Kanuni Rahisi Ambazo Ni Msingi Wa Maendeleo Na Sio Kwamba Tu Hafai Kua Na Maendeleo Ila Anajiletea Umaskini Zaidi.

Kuna Mwajiri Pia Ambae Hataki Kulipa Kodi Wala Kulipa Mishahara Ya Wafanya Kazi Wake Kwa Kigezo Kua Anataka Kutegeneza Faida Kubwa, Binadamu Kama Huyu Hafai Kua Na Maendeleo Na Pale Akijikuta Kafirisika Analaumu Mazingira Bila Kujua Kua Yeye Ndie Mharibifu Pekee wa Mazingira Yake.


Nimetoa Hii Mifano Miwili Kuonyesha Kua Binadamu Siku Zote Ndio Sababu Ya Mazingira Yake.

CHAPTER 3
EFFECT OF THOUGHT ON HEALTH AND BODY

Mwili Ni Kijakazi Wa Akili, Anayefuata Yale Yote Akili Inataka. Bila Kuwa Na Mawazo Mazuri Na Yanayofuata Kanuni Mwili Haraka Hupotea Na Kuoza Katika Mawazo Mabaya

Lakini Katika Matakwa Ya Mawazo Mazuri Na Yenye Furaha, Mwili Unakua Na Muonekano Wa Ujana Na Mzuri Zaidi

Magonjwa Na Afya Ni Kama Mazingira, Mawazo Ya Ugonjwa Hatimaye Hutokea Katika Mwili mawazo ya uwoga yanajulikana kwa kumua binadamu haraka sana kama risasi na yanaendelea kuua maelfu ya watu. mawazo halisi, yenye nguvu, na furaha yanatengeneza mwili mzuri, mwili ni kitu laini ambacho hufuata haraka mawazo,

Mwandishi Anasema Kama Ukiukamilisha Mwili Wako Na Kuilinda Akili Yako Na Mawazo Mabaya Ya Kukata Tamaa, Kuvunjika Moyo Na Etc. Haya Mawazo Huiba Afya Na Utukufu Wa Mwili.

Sura Nzuri Haiji Tu Bali Inatengenezwa Na Mawazo Mazuri,
Namfahamu Mwanamke Wa Miaka 95 Ila Anasura Ya Kisichana Na Kijana Mwenye Sura Ya Mzee Wa Miaka 70

Hivi Karibuni Nimemuona Mwanafalsafa Mmoja Katika Uzee Wake Na Akikaribia Kufa, Hakua Mzee Isipokua Miaka Yake, Alikufa Kwa Amani Na Utulivu Kama Alivyoishi.

Mwandishi Anasema Hakuna Tabibu Mzuri Kama Mawazo Mazuri, Kwa Maana Hukinga Mwili Na Magonjwa, Hakuna Mfariji Mzuri Kama Uwezo Binafsi Kwa Maana Huukinga Mwili Na Kivuli Cha Huzuni Na Msongo.

Mwandishi Anasema Kuishi Katika Mawazo Mabaya Kama Kujikana, Mashaka, Na Tamaa Zilizopitiliza Ni Sawa Na Kujifungia Mwenyewe Katika Gereza.
Bali Kwa Kuyafikiria Vizuri Yote Na Kua Na Tabasamu Katika Yote Na Taratibu Kujifunza Kuona Mazuri Katika Kila Kitu Ndio Njia Pekee Ya Kufikia Amani Ya Moyo.
AS A MAN THINKETH AS A MAN THINKETH Reviewed by Maktaba on September 07, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.