NGUVU ZA AKILI


Kitabu:- Nguvu za akili 
Muandishi:- Justine Bake
Mchambuzi:- Mary Robinson





UTANGULIZI

Muandishi anaanza kwa kusema kwamba, binadamu hutumia 5% - 10% ya akili yake na hii ndio sababu watu wengi huwa hawafurahii Maisha Yao kwa muda mrefu.

Lakini anasisitiza, kuwa zipo mbinu ambazo wengi hawazifahamu ambazo zinafungua vyumba vya ubongo wa mwanadamu Huyu ambavyo hajaanza na wala hajawahi kuvitumia.

Kwa hiyo lengo la kitabu hiki ni kumsaidia mwanadamu ajifunze kutumia hivyo nyumba vingine ili aweze kuishi kwa Raha mustarehe Duniani.

Kitabu hiki kina SURA SABA.

SURA YA KWANZA

(a) Nguvu Za  Akili ni Nini?
(b) Nguvu  za asili ni Nini?
(c) viwango vya akili.
(d) Ni kiwango kipi cha akili huvuta nguvu za asili?
(e)Uhusiano Kati ya akili na ubongo
(f) Akili ni Nini? 
(g) Nguvu Za fikra.

SURA YA PILI
 - Kuhama kiakili (transcendental Meditation)

SURA YA TATU
- Kwa nini tunahitaji kufahamu mazoezi ya kuhama kiakili?

SURA YA NNE
- Mbinu za kuhama kiakili

SURA YA TANO 
- Hatua za kuhama kiakili

SURA YA SITA
(a) Matumizi ya nguvu za akili katika tiba
(b) Matumizi ya nguvu za Akili katika elimu 
(c) Matumizi ya nguvu za Akili katika Kazi

SURA YA SABA
(a) Namna ya kupima kiwango cha Sumu mwilini
(b) Namna ya kuziondoa Fikra hasi akilini
(c) Kanuni za asili na ufafanuzi wake.


SURA YA KWANZA 
Nguvu za akili ni nini?

Muandishi anasema, hakuna kitu kishindacho nguvu za asili. na nguvu za asili zikiingia ndani ya mwili wa binadamu hutenda mambo makubwa na ya ajabu. Muandishi anasema, nguvu za akili ni ule uwezo wa kumuunganisha mtu na nguvu asili. Kwa hiyo nguvu za akili ni lango la kupitishia nguvu za asili ambazo zikipenya mwilini mwa binadamu ambazo zikiingia huleta manufaa makubwa sana kiafya, kiakili na kimawazo.

Muandishi anaendelea kwa kudai kila binadamau ameshawahi kuhisi nguvu za akili zikimwingia mwilini. anatolea mfano, pale ambapo mtu aliwahi kuwazia jambo zuri au kitu akipendacho na akahisi msisimko wa nguvu mwilini mwake. ametolea pia mfano wa pili pale ambapo mtu anaweza akawa amelala amechoka au hata kuwa katika hali ya ugonjwa ghafla akaletewa taarifa nzuri basi ghafla nguvu zikamjia na kuruka bila kujua nguvu hizo zimetoka wapi, basi hizi ndio nguvu za asili. Hii ina ukweli kwa mfano kipindi kile kutokee mabomu Gongolambo, Jijini Dar es salaam kuna watu walitembea hadi posta na maeneo mengine ya mbali, hizi ndio nguvu za asili kwamba hutokea pindi jambo fulani linapotokea liwe la kutisha ama kufurahisha. na nguvu hizi mtu anao uwezo wa kuzitumia kwa kila jambo lake na akafanikiwa, kinachotakiwa ni kujua jinsi ya kuzitumia. na uzuri au ubaya wengi hatujui na hata wanaozijua wengi wamefanya siri kwa manufaa yao binafsi au kundi la watu kadhaa.

Muandishi anasema, nguvu hizo kuponya maradhi na kuleta ustawi wa kiakili kiafya na kimawazo. Kinachotakiwa kujua Ni namna gani ya kuyatengeneza mazingira hayo yavutayo nguvu za asili ili mtu apate afya, maendeleo na Amani ya kudumu.

Muandishi anaendelea kuelezea juu ya nguvu za asili. Anadai kwamba nguvu za asili zimeenea ulimwenguni pote na ndizo hutumika kuendesha/kutendesha Kila kitu kinachofanyika Duniani. Anasema, na nguvu hizi za asili huathiri watu na vitu. Nguvu hizi za asili hazizalishwi na binadamu so kwa jina jingine tunaweza ziita nguvu za Nje.

Anaendelea kwa kusema, binadamu anao uwezo wa kuitumia Nguvu hii ya nje/ya asili pale ambapo nguvu ya ndani haitoshi. Muandishi anasema, mtu yoyote  akiweza kuinasa nguvu hii basi ataweza kuutendesha mwili wake chochote anachotaka.

Mwanadamu anapolala usingizi huvuta nguvu za asili kwa wingi na ndio maana watu wakiamka asubuhi wanakuwa fresh. Uchovu wa Jana unaisha au kupungua. Lakini muandishi anasema nguvu za asili zinazovutwa wakati wa usingizi hazitoshi kuendesha mwili ipasavyo zaidi ya zile zivutazwo pindi mtu anapokuwa ktk hali ya kupata usingizi/nusu usingizi. (Kifupi ni kwamba nguvu za asili humuingia mtu anapokuwa katika hali ya usingizi ama nusu usingizi.

Anasema, kwa kawaida mwili huchoshwa na mihangaiko ya kimaisha na akili inapohangaishwa na mawazo mabaya kama vile chuki, wivu, hasira, wasiwasi, kisirani, woga na mengine mengi yafananayo na hayo na wakati huo huo mtu huyo asipovuta nguvu za asili vya kutosha za kujikarabati mwili Huyu anakuwa kwenye hatari Kubwa ya kupata maradhi ya kufisha km vile presha, sukari,  moyo, kiharusi na anaweza akawa kichaa.

Muandishi anasema, nguvu za asili huvutwa kupitia Akili. Na akili iko katika viwango vitatu.

1.Akili ya fahamu. Hii ni akili ya kwanza ambapo kazi Zake ni kukusanya taarifa zote kupitia milango ya fahamu na huzichuja ndipo hupeleka kwenye akili no. 2 (tutaiona mbele) akili hii hufanya mchakato wa taarifa na kama taarifa hiyo inaonyesha Jambo Hilo lilileta matokeo mabaya Huko Nyuma basi haliziruhusu taarifa hizo kuingia akili no. 2. Halikadhalika akili hii ina uwezo wa kutumia kumbukumbu ilizozihifadhi kwenye akili no. 2 hata siku za baadae na kupata kujua Jambo jema na baya. Na kwa ajili hii ndio maana kuna watu hawawezi badilika wao hung'ang'ania lile lile wanalolijua kwa sababu akili namba Moja haijaruhusu Jambo Hilo kuingia ndani zaidi. (Hapa ndipo unakutaga vita za udini etc, manake akili no. 1 iliruhusu fikra fulani kuingia kwenye akili hizo zingine na kuzitoa ni ngumu)

Anasisitiza kuwa akili ya fahamu huruhusu Mambo mazuri tu kupenya na kuelekea viwango vya juu vya Akili(akili hizo zingine) lakini anasema ubaya wa akili hii ya ufahamu ikiwa Jambo moja litarudiwa Mara nyingi kuizonga akili hiyo basi huruhusu Jambo Hilo kupenya kwenye akili zingine. Na ndio maana hata matangazo ya biashara hurudiwa Mara nyingi na mwishowe hushawishi wanunuzi kuipenda bidhaa hiyo bila sababu kwa sababu imesisitizwa Mara nyingi sana kwenye akili Yao ya ufahamu. Kwa hiyo muandishi anasisitiza kwamba tuepuke kutazama au kusikiliza Mambo tusiyoyapenda kwani yakijirudia sana kwenye akili ya fahamu basi yataingia kwenye akili ya nusu fahamu na kuturudisha nyuma kimaendeleo, kiakili, kiafya hata kimawazo.

2.Akili ya nusu fahamu.

Muandishi anasema, akili hii huchanganua kila taarifa bila kujali Mbaya au Nzuri. Akili hii hulichanganua Jambo kama  lilivyo bila kuongozwa na uzoefu wa nyuma. Na hii ndio Akili ambayo wagunduzi na wabunifu wengi uongozwa nao maana wao hawaathiriwi na kupima jema wala baya (hali ya kusitasita). Anasema, akili hii huleta taswira kama za kwenye ndoto. Akili hii humpeleka mtu kujenga taswira ya kufikirika ya Jambo zuri sana na akiileta kwenye mazingira halisi(ya duniani) basi Jambo Hilo huwa la kuvutia na kusisimua na hapa ndipo wagunduzi hujipatia heshima na umaarufu. Anasema, akili hii huchakata Jambo kwa muunganiko wa maarifa yote kiasi kwamba tatizo lenyewe huwa ni sehemu ya jawabu. Kwa hiyo tofauti kuu ya akili ya fahamu na nusu fahamu ni kwamba akili ya fahamu haitoi suluhisho la tatizo Bali huzuia Jambo baya kuingia kwenye akili ya pili wakati Akili ya nusu fahamu huchakata taarifa bila kuangalia ni Mbaya au Njema na pia hutatua tatizo na kulipatia jawabu. Muandishi anadai kwamba ndio mana watu wanaotumia sana akili ya kwanza hawana uwezo wa kutosha wa kutatua matatizo.

3. Akili ya kutojifahamu.

Muandishi anasema, akili hii haina tofauti na usingizi fofofo ambayo humpeleka mtu kwenye ulimwengu wa vitu visivyoonekana kwa macho na ulimwengu huo ni mkubwa kiasi kwamba ulimwengu huu tunaoishi ni Sawa na punje ya haradali
Na Huko ndiko chanzo ya vitu vyote vinavyoonekana Duniani. Japo vitu hivyo si vya kushikika wala kuonekana ni vitu ktk hali ya mawazo tu. Kama tujuavyo vitu vyote huanza na wazo kabla hakijawa halisi. Basi Huko ndiko penyewe. Na hapo muandishi anashauri kabla ya kulala basi Jenga Tabia ya kujiuliza swali au kitu kinachokusumbua kuwa utakitatuaje etc basi akili hii hulifanyia kazi na kukupatia jawabu siku Moja. Hata kama umetafuta namna ya kufanya Jambo fulani kwa muda mrefu na ukashindwa, muandishi anasisitiza usikate tamaa endelea kufanya zoezi la kujiuliza Mara kwa Mara na siku isiyo na jina utapata jawabu na utashangaa imetokeaje.

Muandishi anasisitiza kwamba hiki ndicho hufanywa na  huwatokea wagunduzi.






NGUVU ZA AKILI NGUVU ZA AKILI Reviewed by Maktaba on September 07, 2017 Rating: 5

3 comments:

  1. The review of this book by R. Robinson is crispy. I couldn't have done better. Karl Marx would have relegated this work to the gallery of metaphysics.Huggin the preacher would have emphasized the immensity of the invisible world and the interaction of the trinity-Body, Soul and Holy Spirit in a person. It is a must read category.

    ReplyDelete
  2. Nisaidie namna kukipata kitabu hiki tafadhari!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.