PEPO YA MABWEGE 

Mwandishi: Dr. Harrison Mwakyembe 
Mchambuzi: Hafidh Kido 
Mpiga chapa: Vide Muwa Publishers Ltd 
Mhariri: Festus J.M.

Riwaya ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 
1981. 
Kitabu kina kurasa 184 na sura 11 zilizoandikwa 
kwa tarakimu za Kirumi kuanzia I hadi XI.

Kwa maelezo ya mwandishi riwaya hii ya PEPO 
YA MABWEGE inazungumzia maisha katika 
jamii, ni riwaya ya kitashtiti inayopinga vikali 
mienendo ya viongozi walaghai na fisadi na 
maofisa wa ngazi za juu wa serikali. 
Washiriki katika riwaya hii Josina na Kalenga 
wanakuwa kwenye mstari wa mbele kukabiliana 
na uongozi mbaya na ingawa wanakumbana na 
changamoto na vikwazo chungu nzima, 
wanafanikiwa kuanika maovu yanayotekelezwa 
na viongozi hao. 
Kwa mkono wake mwandishi anaandika katika 
maneno ya utangulizi: Majina yote yaliyotumika 
katika riwaya hii, ni ya kubuni tu Mathalani, 
mandhari ya kisa hiki na majina ya nchi na 
sehemu, yametumika mithili ya nyenzo ya 
kupigia mbizi katika kisima cha jamii.
Reviewed by Maktaba on September 10, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.