Je, mwanamme wanataka nini? mfumo dume na vuguvugu ukombozi wa mwanamke.
Ni siku nyingine tena na kama ilivyo ada ni kawaida kwa hii safa kuleta mada ambazo ni changamoto kwenye jamii zetu. na lengo ni kuonyesha changamoto iliopo na kutoa suruhu na nini kama jamii tufanye ili kuepuka au kuondokana na hiivita ama mgogoro unaoendelea
so em tuzame sasa katika kitu ninachotaka kukizungumzia leo. unajua duniani saivi kuna vurugu za kutosha na vita zinazozuka kila kukicha ,lakini pia kuna vita za chini kwa chini vita ninayotaka kuizungumzia leo ni ile ambayo ipo chini kwa chini kila mmoja anaijua na labda mda fulani huifikiria kwenye ubongo wake lakini hakuna ambae yuko tayari kulizungumzia swala hili. nazungumzia vita iliopo kati ya mfumo dume na mfumo jike (masculinity and feminism). najua wanaume hawataki kukubali hili lakini ni ukweli usiopingika kua wanawake wa karnr hii ya 21 wanakuja kwa kasi kubwa sana na kuna baadhi ya wachambuzi wa mambo wanadai kua wanaume tusipokua makini kutatokea anguko la mfumo dume (masculinity crisis) na wengine wanadai kua hicho kitu tayari kishatokea na kinaendelea kutokea.
unajua kitu ambacho kinamfanya mwanaume kua mwanaume ni ile hali ya kua mtawala, tegemezi wa familia na kule kuhitajika katika mambo yote muhimu katika jamii na kusimama kama kiongozi lakini sasa mambo yanakua tofauti kidogo wanawake wameamka na wanakuja kwa kasi ambayo hata wanaume hawakuitegemea kutoka kua kama mama wa familia mpaka kufanya kazi ambazo mwanzo zilifikiliwa kua ni za kiume pekee yake na kuingia katika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya familia mpaka ngazi ya taifa.
bila kubisa mfumo dume upo matatizoni na kama hatuta tafuta njia sasa ya kuco-exist kati ya mwanamke na mwanamme na kuwekeana mipaka basi vita hii itakua vita ya tatu ya dunia.
Mpenzi msomaji wangu unajua sio ajabu sasa ukikuta wanawake wakisema kua hawa hitaji mwanamme kwenye maisha yao. kwa maana ile nafasi ambayo mwanamme alikuanayo kama tegemezi wa familia na mtafutaji
Je, mwanamme wanataka nini? mfumo dume na vuguvugu ukombozi wa mwanamke.
Reviewed by Maktaba
on
August 31, 2022
Rating:
No comments: