THE $100 STARTUP: Fire your boss, Do what you love and work better to live more




UKISOMA KITABU CHA "THE $100 STARTUP: *Reinvent the Way you Make a Living, Do what you Love, and Create a New Future"*
By ~ *CHRIS GUILLEBEAU*

Katika kitabu hiki, tunaambiwa kuwa, kuanzisha Biashara ni rahisi sana kiasi cha kwamba unahitaji vitu vitatu tu yaani: bidhaa, kundi la watu na njia ya kulipwa tu! Mambo mengine ni nyongeza tu. Mwandishi anabainisha kuwa, ili kufanikiwa katika Biashara unahitaji ujuzi, kuipenda kazi unayofanya, pamoja na chochote chenye manufaa kwa watu wengine.
Bwana _CHRIS GUILLEBEAU_ anatufundisha kuwa Biashara yenye tija ni ile itakayoendana na uhitaji wa watu, kwahiyo, ni muhimu kuangalia ni bidhaa ipi inahitajika ndipo uizalishe na kila utakapotoa jibu lenye kutatua kero za watu, tegemea malipo maradufu.


Mwandishi anatoa mambo mengi yanayohusu mafaniko katika Biashara, lakini anazidi kusisitiza kuwa, si elimu kubwa ya biashara inayoweza kumpa mtu mafanikio, bali kikubwa ni ufahamu na bidii katika kufanya biashara.
Hiki ni kitabu kizuri sana, hasa kwa wale wanaopenda kujitenga na kundi la wasaka ajira na kuanza mchakato wa kujiunga na “MTANDAO WA WATENGENEZA KAZI” jitahidi ukipate
KARIBU TWENDE KAZI PAMOJA
THE $100 STARTUP: Fire your boss, Do what you love and work better to live more THE $100 STARTUP: Fire your boss, Do what you love and work better to live more Reviewed by Maktaba on January 21, 2020 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.