7 best business book of all the time






Kila mwaka, vitabu vipya vinatoka kuhusu biashara na vinasomwa na watu zaidi ya million duniani kote. Kwa vitabu hivi vingi vinavyotoka kila mwaka, ni ngumu kuchagua ni kitabu kipi ni kizuri na kitanifaa na kipi hakita nifaa.

Hivi karibuni nimesoma vitabu ambavyo watu wengi wanafikiri kua ni vitabu bora katika maswala ya biashara kwa wakati wote.

Hivi vitabu ni vitabu ambavyo vimeandikwa mda mrefu, lakini bado mpaka sasa vinapendekezwa na watu wengi. kama wakosoaji was maswala ya vitabu, watu ambao wamefanikiwa sana katika biashara na pia vipo katika katika new york best seller list. vingine labda tayari unavijua  na umekwisha wahi visoma mwenyew

1. " THINK AND GROW RICH" my Nepolean  Hill

 Wazo kuu: Unaweza kufaikiwa kwenye kitu chochote kile katika maisha kama ukiamini unachokifanya

Mawazo ni vitu, na yana nguvu sana focus katika kitu unachotaka kukifanikisha kua na msimamo na pia ni muhimu kutokukata tamaa kukiwa na changomoto ambazo zinataka kukukosesha unachokitaka.

2. " RICH DAD, POOR DAD" by Robert Kiyosaki 

 Wazo kuu : Jua tofauti kati ya asset na liability. 

Kuna sababu  matajir wanaendelea kua matajir na masikini wanaendelea kua masikini. na sababu hiyo ni kwamba, matajir wanafaham umuhimu wa asset na jinsi gani wanaweza kuzitumia asset hi izo kufund mtindo wao wa maisha. wakati masikini wao wanatumia liabilities kutengeneza mtindo wao wa maisha

Assets, ni vitu ambavyo vinakuingizia pesa mfukoni na liability ni vitu ambavyo vinatoa pesa mfukoni kwako.

3. " THE E-MYTH" by Michael G
erber.

 Wazo kuu: fanya kazi kwenye biashara yako badala ya biashara yako

Watu wengi wanashindwa kuelewa kua biashara na mwenye biashara ni zitu viwil tofauti.  Fanya kazi kwenye biashara yako ili isimame na iweze kujiendesha na kujitegemea yenyewe. biashara ni kama mtoto ambae kipindi yupo mdogo unatakiwa umlishe, umvishe, na kumsomesha ili akikua aweze kujitegemea na kukusaidia wewe

4. " The 22 immutable Laws of Marketing" by Al Ries and Jack Trout

 Wazo kuu: Uuzaji ni vita ya maoni na sio bidhaa
 Katika fani ya uuzaji, kitu ambacho kinaangaliwa sana ni jinsi gani unaielewa bidhaa unayouza . Na uwezo uliona katika kuielezea na ikaeleweka kwa watu na wakakubali kuinunua na sio kua wa kwanza kupeleka bidhaa yako sokoni.

5. HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE  by Dale Carnegie 
Mafanikio ya biashara yako yanategemea sana jinsi gani una deal na watu unaokutananao kila cku. Mwingiliano chanya na watu hupelekea matokeo chanya kwenye biashara yako

6. The Hard Thing About Hard Things my Ben  Horowitz 

 Wazo kuu : Hakuna formula ya kudeal na changamoto katika maisha. 

Ingawa vitabu vingi vimeandika kuhusu challenges tunazopitia katika maisha. Lakini vyote vimeshindwa kutoa definity solution katika kila tatizo ambalo binadamu anapitia. Hivyo, kuacha kua solution pekee ni mtu binafsi


7. The Shoe Dog by Phil Knight 

 Wazo kuu : usimwambie mtu jinsi gani ya kufanya vitu, mwambie nini cha kufanya na atakushangaza kwa matokeo.

Kama hujasoma hiki kitabu tafadhari kitafute kwa maana sio tu kipo kwenye reading list ya bill gate ila kina mawazo mazuri sana ya jinsi gani ya kuweza kuanzisha biashara ndogo na kuimaintain mpaka ikawa biashara kubwa.

Ndani ya hiki kitabu kuna story ya jamaa ambae aliazima dola 50 kwa baba ake ili anzishe biashara ya vitu na akafikia kuanzisha kampuni  ambayo kwa sasa inaingiza 50 billion dollar kwa mwaka


Njia ya kuelekea kweny mafanikio ni kupitia maarifa na maarifa yanapatikana kwenye vitabu


 By Frank Lumato
7 best business book of all the time 7 best business book of all the time Reviewed by Maktaba on January 21, 2020 Rating: 5

3 comments:

Powered by Blogger.