The life and Death of Che Guevara

Kitabu: "Companero"
The life and Death of Che Guevara
Mwandishi: Jorge G. Castaneda 
Mchambuzi: Nanyaro E.J. 
Mhariri: Festus J.M.

Dibaji 

Mwandishi anasema kuwa Che Guevara 
aliishi na kusumbuliwa na pumu(Athma) 
kwa miaka 40,na kwa miezi kadhaa kabla 
ya kifo chake aliishi kwa njaa katika misitu 
mikali huko Bolivia 
Baadae alilazwa katika chumba baridi 
katika hospital ya Nuestra Señora de 
Malta.Anasema Jeshi la Bolivia lilikuwa 
limefanya kosa kubwa sana kukubali 
kumuuza kwa adui shujaa wao,aliyejitoa 
kwa ajili yao.

Miongo kadhaa ya maisha yake Che 
Guevara alikuwa mtu mwenye fikra 
huru,anayependa watu,na mwenye 
utayari wa kupambana msitari wa mbele 
kwa ajili ya wengine.


Chapter 1

CHILDHOOD,YOUTH,AND ASTHMA IN
ARGENTINA

Mwandishi anasema kabla ya anguko kuu
Agerntina ilikuwa nchi nzuri na salama
kuishi,
Ernesto Guevara De Serna alizaliwa
14Juni 1928 Rosario Jiji la tatu kwa
ukubwa likiwa na wakazi 12mil,nchini
Argentina,alizaliwa katika familia ya
Bwana na Bibi Lynch na Celia wahamiaji
ambao walikuwa ni kizazi cha 12 kuishi
huko.Baba alikuwa kutoka Ireland(Mu
Irish) na mama Muhispaniola Babu yake alikimbilia Hispania na baadae Argentina.
Mama yake Che Guevara alikuwa
nguzo.muhimu zaidi kwa Che kabla
hajakutana na Fidel Castro mwaka 1955
nchini Mexico.Mama yake aliugua kansa
miaka 20,Mama yake Che alifariki kwa
kansa,katika hospital ya Buenos Aires
wakati Che akiwa nchini Kongo alikokuja
kuwasaidia Wakongo,Che hakuweza
kutoa heshima za mwisho za mwili wa
mama yake!,aliomboleza kifo cha mama
yake akiwa katika misitu ya Kongo,hata
hivo nae alikuja kufa miaka miwili
baadae. Che Guevara alizaliwa
Njiti(premature),wakati anazaliwa
Wazazi wake walihamia mashambani
kulima chai,hata hivyo kilimo kiliwaendea vibaya hivyo wakahamia jirani na Buenos
Aires ambako baba yake alipata kazi ya
kutengeneza meli,hapo ndio PUMU
ilimuanza Che Guevara mwaka 1930
Mei.Wakati huu wazazi wake walikuwa
wamefilisika kutokana na biashara
kwenda vibaya,mama yake Che akawa na
tabia yanl kujiliwaza mtoni(River
Plate),huko alikuwa anaogelea na yeye
Che akawa anatambaa na kujilowanisha
kwa muda mrefu,ndio maradhi ya pumu
yakaanzia hapo
Mfumo wa kupumua wa Che uliharibika
sana na lawama zote zikawa zinaenda
kwa mama yake mzazi kwa kushindwa
kumwangilia vizuri mtoto wake.Hali hiyo
ilimfanya mama ampende sana Che, na kuanza kumfundisha masomo akiwa
nyumbani jambo ambalo lilikuja
kumfanya Che apende kujisomea vitabu.
Familia hii ilihamahama kutafuta
sehemubya Argentina ambayo ingemfaa
mtoto wao hadi walipofika Alta
Gracia,katika mji wenye hali ya hewa ya
joto ulisaidia hali ya Che kuwa afadhali,wazazi wake walipata watoto
wengine Celia,Ana Maria,Roberto na
Juan Martin.

Mwandishi anasema kuwa Che alisoma
darasa la kwanza hadi la tatu nyumbani
akifundishwa na mama yake,hii ni
kutokana na ugonjwa wa Pumu, alikuja kuendelea darasa la nne shuleni rasmi,ila
ni shule ya kawaida!
Kutokana na Pumu Che alitumia muda
mwingi kitandani na alipojua kusoma
Mama yake alihakikisha kuwa Che
anasoma vitabu mbalimbali ili kumlinda
na upweke(kusoma ni dawa ya
upweke)Baba yake Che alipenda Novels
wakati mama yake alipenda Mashairi kila
mmoja alimletea aina hiyo ya vitabu.
Mwalimu wake alimchukulia Che kama
mtu mwenye akili sana ila asiyependa
kufanya kazi kwa bidii,alikuwa mwanafunzi mwenye kupata wastani wa kawaida,akiwa sekondari alifaulu sana
masomo ya literature na falsafa,somo la
Kingereza alipata 3/10 wakati alifanya
vizuri katika kifaransa akichofundishwa
na mama yake nyumbani. Alipendelea
kusoma vitabu vya washindi wa tuzo ya
nobel ya leterature
Maisha ya wazazi wake yaliendelea kuwa
mabaya hali ya uchumi ikaporomoka kiasi
cha kumfanya Che aanze kufanya kibarua
kwenye kazi za barabarani.Pia migogoro
ikaanza kwenye familia hadi kufikia
wazazi wake kutengana rasmi kama
wanandoa. Che alianza kusoma masomo ya Udaktari huko Buenos Aires.

Chapter 2

YEARS OF LOVE,INDIFERRENCE IN
BUENOS AIRES,MEDICAL
SCHOOL,PERON AND CHICHINA

Mwandishi anasema kuwa mwanzoni
wakati anajiunga chuo kikuu Che alisoma
masomo ya Engineering,lakini ghafla
alibadilisha na kuamua kusoma
Udaktari,kuna sababu tatu zinazoaminika
kuwa zilimbadilisha mawazo Che
Mosi. Kifo cha Bibi yake
kipenzi.Inaaminika kuwa Che alisoma
Udaktari kufuatia kifo cha Bibi yake aliyempenda sana.Bibi yake Che alikufa
kwa ugonjwa wa Stroke na katika moja ya
diary zake Che hiki ni kifo kilichomumiza
sana,hivo akasoma Udaktari ili kuzuia vifo
vya Stroke kwa wengine
Pili.Ugonjwa wa mama yake mzazi
Che,huyu mama alikuwa anaugua kansa
ya ziwa(titi),na alifanyiwa upasuaji na
mwisho ziwa lote likakatwa baada ya
maradhi kuendelea,baada ya ziwa
kukatwa aliugua muda mrefu kwa
maumivu makali.Che aliumia sana kuona
mateso ya mama yake kipenzi,na wengi
wanaamini kuwa inaweza kuwa sababu
ya kusoma udaktari.

Tatu.Ugonjwa wa Pumu.Hoja hii
inakaziwa na yeye Che Mwenyewe
ambaye aliugua ugonjwa huu na baada ya
masomo alifanya utafiti sana kuhusu Aleji
inayosababisha ugonjwa wa pumu na
mfumo wa kupumua kwa ujumla.
Che anasema kuwa wakati anaanza
kusoma Udaktari alikuwa na ndoto za
kuwa Daktari maarufu,na mtafiti maarufu
wa afya,anasema hakuwa kabisa na
mawazo ya kimapinduzi.Anakiri kuwa
ndoto zote hizo zilikuwa kwa ajili ya
utukufu binafsi(personal glory).

Kwa kadri siku zimeenda Che alijikuta
kuwa haipendi tena kazi ya
Udaktari,mwaka 1952 alimwandikia
Mchumba wake Chichina akimwarifu
kuwa hatokuwa tayari kufanya kazi ya
kutibu,badala yake atajikita katika utafiti
zaidi.

Wakati akiwa chuo alikuwa
ameshatembea nusu ya nchi ya Argentina
kwa kutumia baiskeli aliyoitengeneza
yeye mwenyewe.Kusafiri huku akiwa na
rafiki yake Alberto Granado ndiko
kulikombadilisha fikra,mtizamo na
msimamo kufuatia kuona hali halisi ya
umaskini wa watu wake,baada ya
masomo alipata kazi kwenye taasisi moja ya utafiti na kwa nafasi yake ya utafiti
akaweza kusafiri nchi mbalimbali za Latin
America huko ndio aliona jinsi viongozi
wengi wanavyosimikwa na CIA,ambao
walikuwa wanawajibika kwa USA badala
ya watu wa mataifa yao
Kufuatia hali ngumu ya uchumi na
migogoro ya mara kwa mara familia ya
Che ilitengana rasmi kama
wanandoa.Hatua hii ilimuadhiri sana Che
ambaye alikuwa mzaliwa wa kwanza Che ambaye alikuwa mtu mwadilifu sana
aliendelea na mahusiano na binti
Chichina,hata hivo walibusiana kwa mara
ya kwanza baada ya uchumba wao kuwa RASMI.
The life and Death of Che Guevara The life and Death of Che Guevara Reviewed by Maktaba on September 21, 2017 Rating: 5

1 comment:

  1. JFL at Bibi Lynch. She got booted out of the gene pool by her own Chadsexuality, LMAO!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.