DISCOVER YOUR DESTINY

KITABU: DISCOVER YOUR DESTINY.
MWANDISHI: ROBIN SHARMA.
MCHAMBUZI: MADAM.

UTANGULIZI.
Mwandishi nguli wa kitabu pendwa cha "THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI" ambaye ni "ROBIN SHARMA" ametuletea tena moja ya his "master piece". Kitabu kinachoitwa DISCOVER YOUR DESTINY ni kitabu ambacho kina zungumzia jinsi mtu ambavyo anaweza kufikia matarajio yake, Kupata utulivu wa ndani "inner peace", kujitambua "self discovery", na jinsi ya kurudisha na kuboresha mahusiano yetu. Kwa maana mwandishi anasema kuwa,  tumepoteza kabisa mahusiano yetu wenyewe "self relationship" hatujipendi, tunajiona hatustahili kuwa na Maisha mazuri, kuota ndoto kubwa na kuwa na mipango mikubwa ya sisi wenyewe.

Mwandishi anasema kwamba pale tutapofanya hivyo nakuweza kurudisha mahusiano yetu wenyewe utakua mwanzo wa sisi kuishi maisha mazuri na kuweza kuisaidia jamii inayotuzunguka. 

Mwandishi  anasema anasema kuwa huu ulimwengu umejazwa na watu ambao ni fake, maisha yao yote wanaishi maisha ya watu wengine, wanavaa kama watu wengine, na kufanya kila kitu wanachofanya kama watu wengine kitu ambacho kinawafanya mpaka wanakufa bila kujua malengo ya wao kuwepo hapa duniani, kwa maana mwandishi anaamini kuwa kila mtu aliepo hapa duniani ana lengo maalum la yeye kuwepo. Zaidi mwandishi anasema, tumekua na chuki juu yetu wenyewe, hatujikubali vile tulivyo na kwamba makosa tunayoyafanya kila siku ni sehemu ya ukuaji wetu binafsi. Mtu anajichukia kwa kosa alilofanya, halafu anachukia kwanini kafanya kosa kama hilo tena na analichukia kosa hilo. 

Mtu kama huyo kwa kufanya hivyo anakua anabomoa na kuharibu mahusiano yake binafsi, kwa maana tokea hapo anakua hana upendo juu yake tena wala hata kujithamini hajithamini tena na tokea hapo kila kitu atakachokua anakifanya kitakuwa na makosa na pia hakina ubora kwa maana kinakosa muunganiko wa upendo, ubora na thamani iliyoko ndani yake. Ndo maana watu wengi siku hizi hawana amani ya mioyo yao, hawana furaha na kazi zao, ndoa zao na kila kitu anachokifanya kwa maana kila kitu katika maisha yake amekuwa akiambiwa kipi cha kufanya, mke gani aoe, kazi gani afanye na hivi vyote amekua akiambiwa na familia na jamii inayomzunguka.

Mwandishi anasema kuwa kwa kuwa roho inajua sababu ya kuja hapa duniani hivyo huanza kukosa amani na kutokua na furaha hivyo ile hali ya roho kutokuwa na amani na kukosa furaha hujitokeza nje kwa mtu na mtu huyo hukosa furaha kabisa...
DISCOVER YOUR DESTINY DISCOVER YOUR DESTINY Reviewed by Maktaba on September 20, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.