The New Tsar


Kitabu: The New Tsar "The Reign Of Vladimir Putin"
Muandishi: Steven Lee Myers
Mchambuzi: Amani Milando

CHAPTER 24: PUTIN GRAD

Miaka miwili baada ya vita ya Syria kuanza,siku moja bomu la kemikali lilipigwa katika mji mkuu wa Syria,Damascus na kuua watu 1400.Rais Obama aliishutumu serikali ya Rais Assad kwa tukio hilo.huko nyuma Rais Obama aliwahi kusema kua siku ambayo Rais Assad atatumia silaha za kemikali ndio itakua mwisho wa uvumilivu wa marekani na kwamba angeingilia kati na kupeleka jeshi lake kuishambulia Syria.

Kwahiyo lilivyopigwa hilo bomu,Obama akaamuru jeshi la marekani liandae mpango wa kuivamia Syria kijeshi na kufanya mashambulizi dhidi ya Assad.Vladimir Putin yeye,hakufurahishwa na wazo hilo.alimwambia Waziri mkuu wa Uingereza Bw.David Cameron kua hakuna ushahidi kama bomu hilo lilitumika na kama lilitumika nani alilitumia.

Putin na wanadiplomasia wa Urusi waliendelea kushikilia msimamo wa kumtetea Assad na huku wakionyesha wako tayari kumlinda kijeshi.marekani huku akiendelea na maandalizi ya mipango yake na akishawishi nchi washirika wamuunge mkono,mpango huo ulifeli.Uingereza na Ujerumani wote walikataa kuungana na marekani kwenda vitani.Papa Francis pia alimuandikia barua Putin kumuomba ahakikishe mgogoro wa Syria usiishie kwa mataifa makubwa kuivamia kijeshi.mwisho wa siku marekani ikajikuta peke yake,na ikiwa yamebakia masaa machache mashambuliz ya anga dhidi ya Syria yaanze kutoka jeshi la marekani,Rais wa Barack Obama aliufuata mpango huo.

Baadae Obama kwenye mkutano wa G20 aliomba kuonana na Putin na wakakutana wao wawili wakiwa na wakalimani wao tu(sielewi kwanini walitumia wakalimani,maana Putin anajua kiingereza vizuri tu).na wakafanya mazungumzo ambapo Putin alimueleza hakubaliani na mpango wa kuivamia Syria bila kibali cha UN.Ila alimkubalia wazo la kuipokonya silaha hizo za kemikali Syria.kikao kikaisha uvamizi haukutokea tena...
The New Tsar The New Tsar Reviewed by Maktaba on September 27, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.