A Biography of the Africa Continent.

Kitabu: A Biography of the 
                Africa Continent.

Muandishi: John Reader.

Mchambuzi: Nanyaro E.J. 

Mhariri: Festus J.M.

Dibaji. 

John Reader ambaye ni mwandishi wa 
Kitabu hiki ni mtoto wa dereva Tax wa 
Londoni,ambaye alikuja Afrika mwaka 
1955 na kuishi Cape town kwa miaka 
nane kabla ya kuhamia Nairobi alikoishi 
kwa miaka kumi.Akiwa Afrika alifanya 
kazi kama mpigapicha na mwandishi hali 
iliyomfanya awe na uwezo wa kusafiri 
maeneo mengi,anasema aliona mazishi 
ya Tom Mboya na Kwame 
Nkrumah,alishikana mkono(shake hands) 
na Mwl Nyerere,Id Amin,Steven 
Biko,Jomo Kenyata,Ian Smith,Haile 
Selassie etc.

Anasema ana uelewa mkubwa sana wa
mambo ya Kiafrika tofauti na picha waliyo
nayo watu wa Magharibi ambao
wanaona Afrika kama bara giza(dark
continent).
Kitabu hiki kinaeleza ukweli juu ya Afrika
ukweli ambao umefichwa kwa miaka
mingi.Binadamu wa kwanza aligundulika
hapa Afrika kaskazini mwa Tanzania,tena
akiwa ameendelea ni ushaidi wa
ustaarabu wa mwafrika.

Chapter 1

Building a Continent
Mwandishi anasema kuwa bara la Afrika
limeweza kuhimili mabadiliko mbalimbali
ya kijamii,kijiografia,kiuchumi, kuliko
mabara mengine.Miamba yenye umri wa
zaidi ya miaka bil 6 sawa na umri wa
Dunia bado ipo Afrika(miamba iliyopo
Mwanza,na kule Serengeti National
park)Anasema hakuna Bara lingine lenye
muundo huu wa maumbile ya Dunia
tangu uumbaji hadi sasa kama bara la Afrika. Mwandishi anasema kuwa uimara wa
ardhi na miamba ya Afrika,iliyotokana na
miamba hii kubadilika kutoka form moja
kwenda nyingine ndio imesababisha
uwepo wa madini mengi anbayo ni faida
kubwa kwa uchumi wa Afrika.Anasema
Almasi inajitengeneza kwenye hali ya joto
la kati ya 1000-1,150 Degrees!
Mwandishi anasema kuwa uchumi
mwingi wa nchi nyingi za kiafrika kuanzia
wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni
ulijengwa kwa misingi ya madini,nchi
kama Gabon,Ghana,Mali,Siara leone,Zaire,Zambia na Zimbabwe na
Afrika kusini.Ugunduzi wa Almasi huko
Botswana ulifanya uchumi wake kukua
kwa kasi hadi miaka ya 1994.Anaendelea
kusema mkondo(craton) waKaapvaal
pekee una zaidi ya tone 40,000 hadi 1883.

Chapter 2

TRANSITIONS
Mwandishi anasema miaka 3.6 bil
iliyopita mabadiliko ya kimfumo na
kimuundo yalipelekea hadi mimea
kuanza kujitengenezea chakula yenyewe
kupita kwa mfumo wa Photosynthesis,ni
hapa ndio oksijen ilizaliwa
Kufuatia uwepo wa predators(wanyama
wanaokula nyama)Matumizi ya harufu
yalianza ili kuwezesha mwindaji na
mwindwaji kujihami.Hata hivo ongezeko
la wanyama wanaokula nyama lilikuwa muhimu ili wasiishi muda mrefu na hivo
kufa ba kutengeneza rasilimali nyingine
ardhini ikiwepo mafuta na uhai wa
viumbe wengine.
Mwandishi anasema kuwa tafiti
mbalimbali zinaonyesha kuwa mabara
mengine yamemeguka kutoka bara la
Afrika ambalo kwa miaka mingi limebaki
bila kutikisika anasema Human evolution
has been the primary evidence of
supercontinent! anaendelea kusema
Africa is the "keystone of the continental
drift hypothesis".Kwa miaka 200mil
Afrika haijatingishika licha ya uwepo wa
matukio makubwa yanayotishia Dunia
kama Tsunami etc.

Chapter 3

MISSING LINKS
Uwanda wa misitu ya mvua ambayo
imekuwapo kwa miaka 40mil,Sahara
region na Misri ya leo inaaminika kuwa
chanzo cha primates ambao binadamu ali
evolve.Misitu ya kitropical inahifadhi
kiwango kikubwa cha viumbe hai Duniani
Kuna jumla ya aina 4500 za mamalia
Duniani kote huku Afrika ikiwa na
kiwango kikubwa zaidi ya mabara
mengine.Hii ni kutokana na bara hili kuwa Intact na hivyo kuwezesha mabadiliko ya
mara kwa mara ya mamalia.
Mwaka 1735 mwanasayansi wa
Kisweden(swedish) Carl Von Linne
akigundua namna ya kufanya
classfication ndio neno HOMO likaanza
rasmi kutumika.Neno HOMO liliandikwa
kwa kilatin HOMO NOSCE TE IPSUM
tafsiri yake MAN KNOW THSELF..
Hii ilikuwa hatua kubwa sana katika
maendeleo ya binadamu,hasa kutambua
watu kutokana na mahali na eneo.Anasema kuwa kuna dhana mbili
muhimu kuhusu binadamu
1. Kiimani(kidini) wanaaminu katika
uumbaji.
2. Kisayansi binadamu ametokana na
evolution ya Nyani(chimpazee)
aliyebadilika badilika hadi kufikia
tulivo leo(evolution hii
inaendelea)anasema DNA ya Nyani
na Binadamu ina mfanano kwa 99%
ila anakiri kuwa 1%inayobaki ina
maana kubwa sana Miaka milion 200 iliyopita,wakati huo
Dunia ikiwa moja(Pangae) kwa mujibu wa
mwanasayansi Alfred Wegener,
Dinosar(Dinosaurs)ndie mnyama
aliyekuwa anatawala Dunia na alijaa kila
pembe ya Afrika.
Mwandishi anasema kuwa katika bonde
la Fayum lililopo Misri ya leo kuna
ushahidi wa wazi wa maisha ya kale ya.
wanyama wa majini(Reptilia) hasa
samaki,mamba etc...misitu mingi ilijawa na popo.

Chapter 4

ORIGINS AND CLIMATE
Mwandishi anasema kuwa Mabadiliko ya
tabianchi yanaadhiri sehemu kubwa ya
mgawanyo wa makazi ya viumbe hai
Duniani.Lakini hapa Afrika viashiria
vinaonyesha kuwa ushindani wa
rasilimali unaadhiri zaidi ya mabadiliko ya
tabianchi
Mabadiliko ya tabianchi ambayo
tunayashuhudia leo si kwamba yameanza
leo bali yamekuwepo tangu historia ya kijiojia,ndio yaliyosababisha kupotea kwa
Dinosar na ndio yaliyofanya uwepo wa
binadamu!kiumbe hai ambaye
alishindwa kuwenda sambamba na
evolution na adaptation basi kiumbe
huyo alitoweka.
Mwandishi anasema kuwa Bara la Afrika
lilikuwa limeungana na Ulaya likatengana
na baadae miaka mil 16 iliyopita
vikaungana tena na ni kipindi ambacho
kiliruhusu wanyama ambao walikuwa
wanapatikana Ulaya wakahamia upande
ambao ni Afrika na ambao ulikuwa ni
bora zaidi.Mwandishi anasema mgawanyo wa pili ulizaa species
mbalimbali hata ndani ya bara la Afrika
yenyewe.
Anaendelea kusema kuwa Afrika ni
chanzo kizuri na cha uhakika cha taarifa
mbalimbali za kiutafiti wa viumbe hai na
maisha kwa ujumla,kutokana na Uimara
wa Bara hili.Afrika ni maabara ya
mammalian evolution!
A Biography of the Africa Continent.  A Biography of the  Africa Continent. Reviewed by Maktaba on September 13, 2017 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.