FROM THIRD WORLD TO FIRST.


Muandishi:- Lee Kuan Yew
Kitabu:- From Third World To First World 
Mchambuzi:- Sylivanus Kamugisha 

UTANGULIZI
Mwandishi ni Waziri mkuu wa kwanza wa Singapore huru, Lee Kuan Yew, anaelezea safari yake ya kuikomboa Singapore kutoka taifa masikini hadi kuwa taifa tajiri

Lee Kuan Yew.

Alizaliwa mnamo tarehe 16 Sept, 1923, alisomea sheria ktk chuo cha Cambridge na kuhitimu mwaka 1950. Alishiriki kuasisi chama cha People's Action Party mwaka 1954 na alikuwa katibu wake mkuu hadi mwaka 1992. Tangu wakati huo chama cha PAP kimekuwa kikishinda kila uchaguzi kama CCM😀

Singapore Ni Island City State, iliyoko kusini mashariki mwa Asia ikiwa imepakana na Indonesia na Malaysia,  Ina eneo la la km za mraba 719, Inakaliwa na watu 5.6 mil. Ilitawaliwa na Uingereza tangu mwaka 1891 na wakati wa vita vya pili vya dunia ilitwaliwa na Japan kuanzia Februali 1942 hadi Septemba 1945 
Kiuchumi wako vizuri sana GDP yao ni Usd 53,319.
Walipata madaraka ya ndani June 1959, uhuru kamili 31,Augosti 1963, waliungana na Malaysia tarehe16 Sept, 1963, na wakatengana tarehe 9 Agosti,1965.

Wana kituo kikubwa cha biashara cha kimataifa, kituo cha fedha na uwanja mzuri wa ndege, wana bandari kubwa na makampuni ya kimataifa zaidi ya 7000 yameweka viwanda vyao kule, pia ni tax heaven kwa wenye mitaji yao

Mafanikio yote hayo nikutokana na juhudi za mwandishi na timu yake, tutaona ni namna gani walifanya kuweza kufikia hapo. KARIBUNI.

CHAPTER 1: GOING IT ALONE

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa amewahi kusoma vitabu juu ya stadi na maarifa mbalimbali, lakini hajawahi kusoma kitabu juu ya namna ya kuendesha nchi, iliyotokana na mkusanyiko wa wahamiaji kutoka Uchina na maeneo ya jirani

Mwaka 1965 akiwa na miaka 42 alikuwa amekabidhiwa dhamana ya kuongoza watu mil.2, wakati huo baada ya shirikisho na Malaysia kuvunjika, Singapore wakati huo ilikuwa tu na kituo cha kijeshi cha Uingereza pamoja na bandari, ikiwa haina maliasili zozote isipokuwa watu tu

Kulikuwa na changamoto za kiusalama baada ya shirikisho kuvunjika, kwanza hawakuwa na jeshi, jeshi lililokuwepo lilikuwa na makamanda wa Malaysia, pia kulikuwa na wahafidhina waliotaka Malaysia iimeze kabisa Singapore, pia kulikuwa na machafuka ya kikabila hasa baina ya watu wenye asili ya China na Malaysia.
Hata hivyo changamoto kubwa zaidi ilikuwa ya kiuchumi ikiwa na ushindani mkubwa kutoka Malaysia na Singapore waliotaka kuchukua fursa zote za kibiashara na kuiacha Singapore mikono mitupu

Hawakuwa na bara yao(Hinterland) ya kuwapa support na ukosefu wa ajira ulikuwa 14% (kwa sasa ni 1.8%)

Kutokana na changamoto hizo Lee Kuan Yew na timu yake waliazimia yafuatayo;
1. Kuwa ili Singapore iendelee kudumu haitokuwa nchi ya kawaida, kuwa wangejitofautisha kwa kutengeneza bidhaa na huduma kwa njia bora na rahisi zaidi kuliko washindani wao
2. Kuwaamini watu na kuwaendeleza kama rasilimali muhimu zaidi
3. Viongozi waliazimia kuongoza kwa haki na kupiga vita rushwa
4. Matumizi mazuri ya bandari yao iliyokuwa strategicaly located

CHAPTER 2:

BUILDING AN ARMY FROM SCRATCH

Mwandishi anaanza kwa kueleza kuwa wakati wa uzinduzi wa bunge la Singapore hapo Desemba 1965, miezi minne baada ya kujitenga na Malaysia, Brigedia Syed Mohamed Syed Ahmed Alsagoff alimuita na kumweleza kuwa msafara wa kijeshi ndio utampeleka Bungeni, anaeleza kuwa alifadhaishwa na jambo hilo kwa kuwa brigedia huyo mmalaysia alikuwa anajifanya kama ndiye amiri jeshi mkuu

Anaendelea kusema kuwa hali ilivyokuwa kijeshi wakati huo ilikuwa kama vile Malaysia inaitawala Sijgapore

Pia kulikuwa na hali tete ya kiusalama kutokana na machafuko ya kikabila kama tulivyoona hapo awali

Kutokana na hali hiyo alikwenda kuonana na kamishna wa jeshi la Uingereza John Robb na kumwomba asaidie kutuliza machafuko ambapo alikataliwa kwa kuwa eti Uingereza haingeingilia masuala ya ndani ya Singapore.

Kutokana na hali hiyo hawakuwa na namna nyingine isipokuwa kutengeneza jeshi lao na kwa haraka.
Januari 1968 walinunua vifaru vyepesi 73 aina yaAMX 13, kutoka Israel kwa bei nafuu baada ya Israel ku-upgrade silaha zao na Septemba 1969 walinunua magari ya deraya 120 aina ya V200.

Pia walianza kurecruit wanajeshi waliwaendea waingereza na Wamisri wawasaidie kuwafundisha wakakataa , wakawaendea wa Israel wakakubali,

Waisraeli waliingia waki pose kama wamexico ili kuondoa  utata toka kwa waislamu wa Malaysia na hasa wanajeshi,
Walikuja makamanda 18 toka Israel na wakaanzisha mafunzo Novemba 1965

Chini ya mwongozo wa makamanda wa Israel, kukaanzishwa vikosi kadhaa lakini hasa mpango mkubwa wa jeshi la kujenga taifa ambapo kuanzia viongozi hadi wakulima walitakiwa kupata mafunzo ya kijeshi. Kwa hiyo kukawa na jeshi dogo la kambini na jeshi kubwa la akiba uraiani

Hadi kufikia 1970 walikuwa na batalian 31 wakiwa pia na vikosi vyote muhimu mpaka na unit ya makomandoo . Waingereza walitangaza kuondoa vikosi vyao 1971 hivyo kukawa na ulazima wa kuanzisha kikosi cha wanamaji kwa ajili ya ulinzi wa pwani pamoja na kikosi cha anga

Ili kuongeza morali tangu mwaka 1971 kulikuwa na mpango wa kuwachukua best officer cadets kwenda kusoma nje ya nchi katika vyuo vikuu kama Harvad au Stanford kozi za Uongozi, uhandisi n.k na wakirudi wanatumikia jeshi kwa miaka 8, baada ya hapo wanachagua kuingia serikalini au sekta binafsi

Kutokana na udogo wa eneo lake jeshi la Singapore imebidi liwe na vituo nje ya nchi kama Taiwan, Australia na Marekani, jeshi hilo ni la kisasa kabisa likitumia 4.9% ya pato la taifa kiwango ambacho ni kikubwa kabisa katika ukanda huo.

:CHAPTER 3:
BRITISH PULLS OUT

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa uwepo wa jeshi la Uingereza katika Singapore imani kuwa wasingeweza kushambuliwa kirahisi na maadui zao, pia uliwapa wananchi hisia za kuwa walikuwa salama, lakini pia wawekezaji walikuwa na uhakika  wa usalama wa mitaji yao

Januari 1966 mwandishi alionana na waziri mkuu wa Uingereza wakati huo Harold Wilson ktk mkutano wa jumuiya ya madola mjini Lagos akamweleza kuwa Uingereza ingepunguza majeshi yake katika Malaysia na Singapore kutoka 50,000 hadi 25,000.

Ili kupata uhakika mnamo Aprili 1966 alienda Uingereza ili kujadiliana nao kwa kina kuhusu masuala ya usalama ktk kusini mashariki mwa Asia.
Alikutana na Denis Harley, waziri wa ulinzi ambaye alimwambia kuwa Uingereza ingeondoa majeshi yake Singapore ktk kipindi cha miaka 5

Hofu yao nyingine kuhusu kuondoka kwa majeshi ilikuwa kwa sababu jeshi la Uingereza lilikuwa limeajiri watu zaidi ya 30,000 hivyo walikuwa na hofu ya ukosefu wa ajira kwa watu wao

Baada ya kuwa ameondoka Uingereza mwandishi anasema Wilson alipata shinikizo sana kuhusu kupunguza matumizi ya kijeshi nje ya Uingereza, bunge la Uingereza likawa linataka kuondoa majeshi mapema zaidi mwaka 1971 badala ya 1975

Baadaye waziri wa ulinzi Harley alitembelea Singapore na kueleza kuwa uamuzi wa kuondoa majeshi ni kwa sababu za kiuchumi na haungeweza kubadilika.
Baadaye mwandishi alirudi tena Uingereza kwa Mwaliko wa Wilson kwenda kuhutubia mkutano wa mwaka wa chama cha Labor ambacho kilikuwa na mrengo sawa na PAP Yaani Social democrats akajaribu tena kuomba majeshi yabaki ktk eneo lao kwa kuwa eti nchi yao ndio ilikuwa haifuati ukomnisti na kuwa ingeweza kusumbuliwa na China. Juhudi zote hazikufanikiwa

Baada ya kuona hakuna namna nyingine ya ushawishi zaidi waliomba kuwa Mitambo na vifaa vya kijeshi visiharibiwe bali viachwe ili vitumike kijeshi au kiraia

Waliomba dock yard ya Keppal na Sembawang waibadilishe iwe ya matumizi ya kiraia na walipata mwekezaji, kampuni ya  Swan & Hunters ambayo ilitumia kutengenezea meli za kiraia

Mnamo Juni 1970 chama cha Conservative  kilishinda ktk uchaguzi huko Uingereza na Edward Heath alichaguliwa kuwa waziri mkuu, hata hivyo mpango wakuondoa majeshi uliendelea kama kawaida. Hivyo ilibidi Singapore wakubaliane tu na hali halisi na kujizatiti kiulinzi wao wenyewe.

CHAPTER 4:

SURVIVING WITHOUT A HINTERLAND

Katika sura hii mwandishi anasema baada ya kujiondoa ktk shirikisho na Malaysia na kuondoka kwa majeshi ya Uingereza, walikuwa wameondolewa sifa na umaarufu wa kuwa kituo kikubwa cha utawala na kituo kikubwa cha dola ya Uingereza ktk kusini mashariki mwa Asia

Anasema alikutana na mshauri  wa uchumi kutoka Uholanzi Dr. Albert Winsemius ambaye alishauri kuwa Singapore ipenyeze bidhaa na huduma zake katika soko la Marekani, UK, Australia na New Zealand

Winsemius alishauri kuwa wanahitaji wawekezaji wakubwa kutoka Amerika na Ulaya.

Kwanza waliunda bodi ya utalii, na kumteua Runme Shaw kuwa mwanyekiti

Pia walihakikisha wanaanzisha viwanda, japo soko lao lilikuwa dogo la watu mil.2, walilinda bidhaa zilizokuwa assembled ndani kama magari, majokofu, Ac, redio nk. Kwa kutegemea kuwa baadae zingeweza kutengenezwa moja kwa moja ndani.
Waliwapa motisha na nafuu ya kodi wafanyabiashara wa ndani walioweza kuanzisha viwanda vidogo vidogo

Kwa kutumia majengo yaliyoachwa na jeshi la Uingereza wakatengeneza viwanda vya aina mbalimbali,

Waliunda Bases Economic Conversion Board chini ya ofisi ya waziri mkuu ili kuajiri upya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi katika makambi ya kijeshi na kuchukua ardhi na amana nyingine za majeshi ya Uingereza, ikawa kwamba wafanyakazi wakaajiriwa ktk viwanda vipya vilivyoanzishwa.

Katika majira ya joto 1968 Lee Kuan Yew alichukua likizo ya mafunzo (sabbatical) katika Kennedy school of government , Harvard. Akajifunza kuhusu Marekani, akajifunza kuhusu teknolojia, masoko, viwanda nk. Akakutana na watendaji wa Makampuni makubwa ya Marekani. Baadaye Novemba 1968 alienda New York na kukutana na watendaji 800 ktk Economic Club of NY.

Baadaye wakaamua kuwa wawavutie Multinational corporations ( MNC), hasa ya Marekani.
Kwa kuwa MNC walikuwa wanalwta teknologia kubwa na ya kisasa na wanaajiri watu wengi

Hivyo wakawa wameamua kuwa watakuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa bidhaa za MNC ili kuuza katika nchi zinazoendelea.

Wakaachana na dhana ya wakati huo kuwa MNC Ni mashirika mumiani ya kunyonya rasilimali na kuendeleza ukolono mamboleo.

Walichojali ni kuwa walitaka watu wao wapate ajira, na maisha mazuri

Walianzisha Economic Development Board kama one stop centre kwa wawekezaji. Pia ilikuwa na jukumu la kwenda nje ya nchi kuvutia wawekezaji.

Hadi mwishoni  mwa 1970 makampuni makubwa kama Texas Instruments, HP,na mengine yakawa yameweka viwanda vyao Singapore na mpaka 1997 makampuni 200 ya Marekani yenye jumla ya thamani ya zaidi ya $ 20 bil.

CHAPTER 5:

CREATING A FINANCIAL CENTRE

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa mwaka 1965 walipotengana na Malaysia, hakuna mtu angedhani kuwa Singapore ingekuwa na kituo kikubwa cha kifedha kimataifa

Anasema ilianza kama utani kwa Dr. Winsemius ( yule mshauri wa uchumi) kumpigia simu rafiki yake Van Oenen aliyekuwa VP wa Bank of Amerika tawi la Singapore na kumueleza kuwa Singapore ingetaka kuwa na Financial centre ktk kipindi cha miaka 10, Yula bwana akamualika Dr. Win London na kumwambia kuwa wanaweza kupata kituo ktk kipindi cha miaka 5,

Akamuelekeza kuwa shughuli za Vituo vya kimataifa vinaanzia Zurich wakimaliza wanatuma taarifa Frankfurt, baadae London, baada ya London inafuata New York baada ya NY inafuata San Fransisco, San Fransisco wakifunga kunakuwa na gap la muda kabla ya Zurich kufungua tena Hivyo Singapore wakiweza kuwa na Financial Centre ingefanya kuwa na huduma kwa masaa 24 bila kusimama.

Kwa kuwa Singapore ilikuwa Dunia ya tatu wakati huo, ilibidi wawe na miundombinu bora, hali bora ya huduma pamoja na wataalamu wa kutosha ili kuvutia Benki za Nje

Pia ilibidi wazishawishi benki za nje kuwa Bodi ya sarafu na Mamlaka ya Fedha zilikuwa na uwezowa

Uwezo wa kudhibiti sekta ya mabenki. Mamlaka ya Fedha(Monetary Authority of Singapore- MAS) Ilikuwa inajitahidi kuweka udhibiti  kulingana na sheria na taratibu ili kujenga confidence kwa wawekezaji

Walianza na Asian dollar market  ambayo ilikuwa baina ya mabenki ndani ya Singapore yaliyokuwa yakipata fedha toka nje kwa ajili ya mikopo baina ya mabenki nk. Hadi kufikia 1997 Asian dollar market ilikuwa na mitaji ya jumla ya  $ 500 bil.

Misingi ya mafanikio yao kifedha ilikuwa sababu ya utawala wa sheria, na serikali imara ya kuaminika
Kwa usimamizi wa MAS Ilishairi benki nne kubwa kuungana na benki ndogo na kuzifanya imara zaidi
 Baada ya kutoka madarani kama waziri mkuu, alipata muda wa kuangalia sekta ya fedha akiwa nje na kuona mapungufu, kuwa sekta ilikuwa inaangalia ndani zaidi na si nje, badala yake wangeweza kuongeza control ya mfumo

Hivyo kwa kuitimia MAS walifanya mabadiliko kwa kuongeza watu wenye uzoefu kutoka Marekani maeneo mengine yenye wataalam, na kwa hivyo sekta ya fedha ikawa imechangamka.

CHAPTER 6:

WINNING OVER THE UNIONS

Mwandishi anaanza kwa kueleza kuwa alianza maisha yake ya kisiasa kwa kupitia vyama vya wafanyakazi

Hadi mwaka 1950 wakomunisti walikuwa wamechukua hatamu za uongozi ktk vyama vya wafanyakazi na ambao migomo ndo ilikuwa staili yao ya kudai haki

Mwandishi amasema kuwa Julai 1961 hadi Septemba 1962 kulikuwa na migomo 153 katika . Ila mwaka 1969 hakukuwa na mgomo wowote, je walifanyaje kufikia hali hiyo?

Kwanza baada ya Uingereza kutangaza kuondoa majeshi, umma ulipatwa na taharuki kuwa wangepoteza ajira na hivyo kipato.
Mwandishi anasema aliwaita viongozi wa vyama vya wafanyakazina kuwaeleza kuwa wakoloni wameondoka hivyo kilichobaki ni kufanya kazi bila kudeka kama walikuwa wanataka maendeleo

Aliwaeleza kuwa kila mwaka watu 30,000 walikuwa wanaingia ktk soko la ajira, na pia wawekezaji wangeleta mitambo mikubwa hivyo kupunguza wafanyakazi

Kwa huyo walibadilisha mindset na namna ya kupima uzalishaji kuwa watu walipwe kulingana na uzalishaji na siyo kuhudhuria kazini

Vilevile kupitia kampeni mbalimbali viongozi waliendelea kuwaelekeza wafanyakazi kuhituma na kuzalisha zaidi na serikali pamoja na waajiri binafsi walitakiwa kuongeza mafao ya wafanyakazi

Aprili 1968 ilipitishwa sheria ya Ajira na Vyama vya wafanyakazi ambapo, sheria na taratibu za ajira,likizo, overtime,maternity,nk.
Pia waliainisha uwezo wa mwajiri kuajiri na kuachisha kazi (Hire and Fire)
Vilevile ilipitishwa kuwa Chama cha wafanyakazi kisingeitisha mgomo hadi ipigwe kura ya siri vinginevyo viongozi wangeshtakiwa.

Vile vile ziliundwa bodi za ushauri na usuluhishi ili kulinda haki za vyama, wafanyakazi na Serikali.

CHAPTER 7:

A FAIR, NOT WELFARE, SOCIETY

Mwandishi anasema kuwa waliamini katika ujamaa,  kuwa kula mtu angepata stahili yake, kwa kuwa watu wana vipawa na uwezo tofauti, kama utendaji na tunzo(reward) vitategemea tu nguvu ya soko, basi kunakuwa na washindi wachache, wa-kati kiasi na malofa  kibao. Anasema hali hiyo inasababisha wasiwasi (tension) kijamii.
kuweka usawa wa kijamii na kuondoa madhara ya uchumi wa soko mwandishi anasema kuwa waligawa keki ya taifa kwa vitu ambavyo vingeongeza uwezo wa watu kama Elimu, Nyumba na Afya

Kipaumbele cha mwandishi na timu yake ni kuwa kila familia iwe na nyumba

Septemba 1963 baada ya uchaguzi iliundwa Housing and   Development Board ili kujenga nyumba za gharama nafuu kwa wafanyakazi na wafanyakazi wangelipia 20% advance na kulipia kidogo kidogo kwa miaka 15.

Serikali ya kikoloni ilikuwa imeanzisha  Central Provident Fund kama mfuko wa mafao ya wastaafu ambapo wafanyakazi walikatwa 5% ya mshahara na asingeweza kuchukua mpaka adikishe miaka 55.

Mwandishi anasema walirejea sheria ya CPF kwa kuongeza makato na kuweka mpango kuwa mfanyakazi angeweza kutumia mafao yake kulipia 20% advance ya nyumba na kuendelea kulipia kidogo kidogo mpaka deni litakapoisha. Kutokana na mpango huo watu wengi wakafanikiwa kuwa na nyumba na kulingana na mabadiliko ya kipato wakawa wanahama kulingana na uwezo wa kipato. Serikali ilibadilisha sheria na kutwaa ardhi ambayo ilikuwa haijaendelezwa na kuendelea kujenga nyumba.

Eneo jingine ambalo mwandishi anasema walitilia mkazo ni huduma za afya, walianzisha mfuko wa Medisave ambapo CPF ilikuwa inakata pesa ktk michango ya wafanyakazi na kuingiza ktk mfuko huo kwa ajili ya matibabu

Baada ya CPF kuwa na mtaji mkubwa Walianzisha uwekezaji ktk vitegauchumi vingine kama Mabasi, nk

Mwandishi anasema sera zao zilisababisha ulinganifu wa kifedha na kuwa na ziada , tangu 1960 walikuwa ma ziada ya bajeti yao na matumizi ya serikali ni 20% ya pato la taifa

CHAPTER 8:

THE COMMUNISTS SELF DESTRUCT

Mwandishi anaongelea chama cha upinzani cha kikomunist kilichojulikana kama Barisan Sosialis

Katika uchaguzi wa Septemba 1963 chama hicho kilipata viti 13 kati ya 51 na asilimia 33 ya kura na kikawa chama kikuu cha upinzani.
Wakati Singapore ilipotengana na Malaysia, mwenyekiti wa Barisan Sosialis Dr. Lee Siew Choh aliudhihaki uhuru wa Singapore na kuuita wa kimamluki. Akasema kuwa wasingeshirikiana na serikali ya namna hiyo.

Akaitisha maandamano ya wafuasi wake nchi nzima lakini yakazimwa na polisi.
Wabunge wa chama chake wakajiuzulu na uchaguzi ukarudiwa, uchaguzi uliporudiwa chama cha PAP Kikachukua viti vyote.

Katika uchaguzi wa Januari 1968 Barisan Sosialis walisusia uchaguzi PAP Ikachukua viti vyote na kikapata 80% ya kura zote

Wakomunsti walikuwa wanawashawishi raia kuwa mapinduzi ya kijamii ya Mao ktk China yangeendelea ktk Asia yote na kuwa Ukomunisti ndio itikadi ya kudumu. Mwandishi anasema baada ya Wakomunisti kushindwa ktk sanduku la kura waliunda vikosi vya kigaidi na kukimbilia kusini mwa Malaysia.

CHAPTER 9:

STRADDLING THE MIDDLE GROUND

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa tangu mwaka 1959 chama cha PAP Kimeshinda chaguzi 10 mfululizo katika kipindi cha miaka 40, Je ni kwa sababu gani?

Anasema ushindi wao daima haukuwa wa mtelemko, daima ulikuwa wa mapambano ya nguvu,
Kwanza walikuwa wakipambana na wakomunisti, halafu Malaysia ilikuwa imedhamiria kuwameza. Anasema matukio hayo na mengine mengi yalijenga imani ya wapigakura  kwa chama cha PAP

Anasema wapinzani wao walikuwa wakidai kuwa PAP kilibaki madarakani kwa kukandamiza upinzani jambo ambalo si kweli, ukweli ni kuwa PAP ilibeba ajenda ya maendeleo ya wananchi

Anasema haikuwa kazi rahisi kuitoa Singapore ktk umaskini hadi utajiri katika kizazi(generaation) kimoja

Anasema pamoja na kuwa walikuwa wakishainda kuna kama 20% ya watu hawakuwachagua yaani kulikuwa na maeneo ya wapinzani, badala ya kuwapuuza anasema walipelekewa miradi ya maendeleo kuliko hata sehemu ambazo walikuwa wakiungwa mkono

Mwandishi anasema sera za PAP za kujenga nyumba na kuwamilikisha wananchi, huduma bora za afya na elimu bora viliwafanya watu wengi wajione sawa na waipende serikali yao

Mwandishi anasema alikuwa hawezi kuvumilia kashfa na tuhuma ambazo si za kweli dhidi yake na mara alipotuhumiwa isivyo alienda mahakamani ambapo kama ilionekana amekosea alilipa fidia hivyo hivyo kwa washindani wake. Amewahi kuyashtaki na kushinda magazeti ya Utusan Melayu la Malaysia na International Herald Tribune la marekani

Anasema baada ya PAP Kuongoza kwa muda mrefu ilionekana kama vile bunge limekosa mvuto kwa kutokuwa na hoja kinzani, hivyo mwaka 1990 waliweka sheria ya kuwepo wabunge wa kuteuliwa kutoka asasi za kijamii, ambapo bàada ya hapo uhai wa bunge na mijadala mikali imekuwepo.

CHAPTER 10:

NURTURING AND ATTRACTING TALENT

Mwandishi anaanza kwa kusema usiku wa tarehe 14 Agosti 1983 wakati akilihutubia taifa kwa njia ya redio na TV Alilipua bomu pale aliposema kuwa ilikuwa ujinga kwa mwanaume msomi kuoa mwanamke ambaye hajasoma kama wanataka watoto wao wafanye vizuri ktk masomo yao.
Anasema wanawake walikasirika sana eti kawaita Vilaza na kwa hasira anasema mwaka uliofuata wakati wa uchaguzi chama chake kilishuka kwa 12%

Anasema kulikuwa na tatizo la kijamii ambapo graduates wa kike ambao walikuwa kwa idadi sawa na wa kiume walikuwa hawaolewi sana yaani chini ya theluthi moja, wanaume wakipendelea kuoa wanawake wa elimu ya chini yao.

Anasema kilichomtuma kutoa hotuba hiyo ni kuwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 1980 ilionesha kuwa wanawakecwasomi walikuwa hawaolewi na wasingewakilishwa ktk kizazi kijacho. Anasema aliamua kusema hivyo ili kuwastua wanaume wàache ujinga na waoe wasomi wenzao

Kwa kubuni mbinu mbalimbali kama kutoa unafuu wa kodi kwa wanawake graduates walioolewa hatimaye hali ilibadilika kidogokidogo. Anasema hadi kufikia 1997 graduates walioa graduates wenzao kwa 63% ukilinganisha na 38% ya mwaka 1982

Anasema tangia mwaka 1970 Singapore ilianza kukumbwa na brain drain ambapo 5% ya wasomi wao wazuri walianza kuhamia nchi nyingine

Anasema mwaka 1980 waliunda kamati ya kutafuta na kuhifadhi vipaji ambapo wqlienda mpaka Marekani kutafuta Asian best students na kuwaahidi kazi zenye maslahi ktk Singapore, kwa waliokuwa vichwa zaidi walipewa hata ajira na kula kabisa mshahara wakiwa bado wanasoma.

CHAPTER 11:

MANY TONGUES, ONE LANGUAGE.

Mwandishi anaanza kwa kusema yeye na mke wake Choo😆 walisomea katika shule za kiingereza

Anasema wakati Singapore wanaunda serikali mwaka 1959 waliamua kimalay kuwa lugha ya taifa ili kujiandaa kwa kuungana na Malaysia. Baadae waliona kuwa kiin.gereza ni muhimu kwa sehemu za kazi na biashara. Kama eneo la biashara la kimataifa hawangefika mbali kwa kutumia kichina, kimalay au kitamil

Wazazi wengi wenye asili ya China walipenda sana utamaduni wao na kuwa watoto wao wasomee kwenye shue za kichina, hivyo hivyo kwa watamil na wamalay. Kwa hiyo kulikuwa na mgongano baina ya makabila kila moja akitaka lugha yake ndo itumike

Hivyo ili kuondoa tofauti hizo mwaka 1975 ikawa  kwamba shule zote mpaka vyuo watumie kiingereza


CHAPTER 12: KEEPING THE GOVERNMENT CLEAN

Mwandishi anaanza kwa kueleza kuwa chama cha PAP kilipoingia ofisini mwaka 1959 waliazimia kuwa na serikali safi, tofauti na ilivyokuwa katika nchi nyingine ktk Asia.
Serikali ya Lim Yew Hock (1956 - 1959) ilikuwa na ufisadi kuna mawaziri walikuwa wanapokea rushwa kutoka nchi za nje na jambo hilo lilisaidia PAP kushinda 1959.

Anasema kulikuwa na vishawishi kila mahala vya kuchukua rushwa; polisi barabarani, hospitalini, nk.

Anasema walipochukua nchi mwaka 1959 waliazimia kuwa fedha zote za serikali zitatumika kwa matumizi halali bila kufisidiwa.
Walibadilisha sheria ya Corruption Practices Investigation Bureau (CPIB) iliyokuwa imetungwa na wakoloni kushughulikia rushwa ndogo,ili iweze kushughulikia ufisadi mkubwa.
Sheria mpya iliipa CPIB mamlaka ya kuchunguza,kukamata, na kupeleleza mpaka akaunti za watuhumiwa, wake na watoto wao, pamoja na mawakala wao.
Ushahidi ungeweza kuwa tu kuwa mtuhumiwa anaishi maisha ya juu  tofauti na kipato chake halali.

Vile vile mwaka 1989 waliongeza faini ya juu ya makosa ya rushwa kutoka S$10,000 hadi S$ 100,000, na kutoa ushahidi wa uongo faini hadi S$ 10,000 pamoja na kifungo.
Baada ya hapo kesi kubwa za ufisadi zilianza ikiwemo ya Tan, Kia Gan waziri wa Maendeleo ya taifa, mwaka 1960 na Wee Toon Boon waziri wa Mazingira mwaka 1975 wote walipatikana na hatia na kufungwa

Mwandishi anasema kanuni moja kuu ya serikali safi ni kutokutumia fedha kushinda uchaguzi, anasema serikali ya PAP haikutoa zawadi au pesa zozote ktk kampeni zake, isipokuwa ahadi za kuwaletea wananchi maendeleo na ambazo ilikuwa ikizitimiza.

Anasema mwaka 1970 mshahara wake ulikuwa wazi S$ 3,500 na mawaziri S$4,500, baadae uchumi ulivyokuwa unaimarika na mishahara yao inapanda sawia

Anasema Singapore ni nchi ya saba duniani kwa uwazi na kutokuwa na rushwa.

CHAPTER 13:
GREENING SINGAPORE

Mwandishi anasema baada ya uhuru  alitaka Singapore iwe tofauti na nchi nyingine za dunia ya tatu. Na kitu cha kwanza rahisi aliona ni kuwa na nchi safi na ya kijani.

Anasema kujenga miundombinu ilikuwa rahisi, lakini kubadili mindset za watu ilikuwa shughuli kubwa.

Anasema miaka ya 60 kulikuwa na machinga waliokuwa wanauza bidhaa mitaani, mama ntilie wakiuza chakula kil mahala, taxi bubu nk. Shughuli zote hizo zilifanya mji kuwa mchafu. Pia watu waliishi katika makazi duni(slums)

Anasema baada ya kuanza kutekeleza sera ya kila familia iwe na nyumba, taratibu hali ilianza kubadilika, pia kutokana na kufunguliwa kwa viwanda , watu wengi walianza kupata ajira nzuri na kuachana na uchuuzi wa mtaani. Vilevile wale ambao hawakuwa na namna waliwekewa sehemu zao wakapewa mabanda wakasajiliwa na kufanya shughuli zao kwa ustaarabu zaidi

Anasema alianzisha kampeni ya kupanda miti, na akaunda idara ya kutunza miti katika wizara ya mazingira. Mwaka 1971 walianzisha siku ya taifa ya upandaji wa miti. Na tangu wakati huo kila mwaka kuanzia viongozi mpaka wananchi wanapanda miti.

Pia wanafunzi wa shule kila mmoja lazima awe na mti wake.
Anasema alitafuta watalamu wa udongo kufanya utaafiti wa udongo na aina ya miti na maua na nyasi zinazoweza kustawi ktk nchi na wamefanikiwa kuifanya nchi hiyo kuwa ya kijani

Pia walianzisha Anti- pollution unit ambayo inashughulika na kudhibiti uchafuzi wa mito na bahari kutokana na taka za viwandani nk.
Mwaka 1971 waliunda Monument Preservation Board kwa ajili ya kulinda urithi wa majengo ya kale na kazi za sanaa pamoja na minara
Pai mwaka 1970 walipiga marufuku matangazo ya sigara na kuanzisha "smoke free week".
Kuanzia mwaka 1992 wamepiga marufuku Big G😆😆

CHAPTER 14:
MANAGING THE MEDIA

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa vyombo vya habari vya Singapore vilianzishwa na wanahabari wa kikoloni kabla ya uhuru mwaka 1959
Anasema ilichukua muda mrefu kabla ya kizazi kipya cha wanahabari kugundua kuwa kuna mwelekeo mpya, na kuwa siasa na utamaduni wa Singapore ni tofauti na ule wa Magharibi

Anasema namna ya kuwasilisha taarifa katika vyombo vya habari vya kimagharibi imetawaliwa zaidi na kupingana na mamlaka na mifumo, wakati ktk Asia wanahabari wanaripoti kwa kupongeza na kukubaliana na sera na mamlaka za kiutawala

Anasema katika Singapore, kuna jamii mbalimbali kama watu wenye asili ya China, Tamil, Malaysia, Uingereza, na wa lugha nyingine mbalimbali.
Kutokana na hali hiyo ilibidi kuwa na magazeti ya kiingereza na kilugha ili kukidhi mahitaji ya kila upande hasa kabla ya kufanya kiingereza kuwa lugha ya kufundishia.

Anasema Kulikuwa na magazeti ya Straight times la kiingereza, Nanyang Siang Paw la kichina, Utusan Melayu la kimalay nk.

Kama tulivyoona awali mwandishi na timu yake hawakuvumilia kashfa kwa kuwa ni mambo ya kisiasa, walipambana na yeyote na chombo chochote kilichowashambulia aidha kwa kulitaka gazeti liombe radhi, kwa kwenda mahakamani au kwa kutumia mamlaka.

Anasema kulikuwa na gazeti moja kubwa na Straits Times la Waingereza, lakini ili kuongeza ushindani walishawishi watu waanzishe magazeti na yalianzishwa magazeti kama Singapore standards mwaka 1960 na Eastern Sun mwaka 1966. Anasema walikuwa wanachunguza kuwa magazeti hayatumiwi na maadui wa nje kuleta chokochoko za kisiasa nk. Kama walivyogundua gazeti la Singapore Herald lililoanzishwa mwaka 1970 na wamarekani kumbe walikuwa matapeli.
Mwandishi pia anaeleza kuwa hata kwa magazeti ya kimataifa iwapo yangeripoti habari isiyo ya kweli yalibanwa kama ilivyotokea kwa Asian Wall Street Jounal Disemba1986, Far Eastern Economic Review Disemba 1987.

CHAPTER 15:
CONDUCTOR OF AN ORCHESTRA

Mwandishi anaanza kwa kusema kuwa yeye na timu yake ni watu ambao walikuwa wamefahamiana kwa muda mrefu sana, wengine mpaka shule za sekondari walikuwa wamesoma pamoja.
Kwa hiyo anasema utendaji kazi wake haukuwa mgumu, wala hakupata shida kuumgwa mkono katika ajenda zake.

Anasema kuendesha serikali si sawa na kuimbisha kwaya(conducting an orchestra). Amaseka hakuna kiongozi anayeweza kufika mbali bila kuwa na timu mahiri. Anasema katika teuzi zake alikuwa akichagua watu mahiri kwa kadri ilivyowezekena.

Miongoni mwa mafanikio ambayo mwandishi anayaelezea ni pamoja na:

SINGAPORE AIRLINES AT CHANGI AIRPORT

Mwanzoni walikuwa na ubia na Malaysia wakiwa na shirika liloitwa Malaysia-Singapore Airlines(MSA) lakini walitengana 1972 na Singapore ikaanzisha Singapore Airlines (SIA), anasema walipata shida kushindana na mbia wao wa zamani Malaysia ambayo alikuwa kama ndiye mmiliki wa ruti zao za zamani wakati wa MSA. Hata hivyo anasema ilividi wapambane kupata ruti kama za Hong Kong, Tokyo, Sidney, Jakarta na Bangkok. Anasema walikuwa wamezuiwa kupata kibali cha kutua London mpaka walipoifanyia mgomo ndege ya Uingereza ambapo ilipotua wafanyakazi hawakushughulika nayo mpaka balozi wa Uimgereza akaenda kumuona, naye akamwambia awaambie wenzake watende haki. Wiki moja baadae walipata ruti. Wakaanzisha ruti ya London-Singapore-Sydney
Anasema wakati wa uzinduzi wa SIA aliwaambia watendaji kuwa SIA ilipaswa kujiendesha na si kubeba tu bendera na kuwa iwapo ingepata hasara angeifunga mara moja.
Anasema hadi 1996 SIA inamiliki ndege bora kabisa aina ya Airbus na Boeing na ni shirika la ndege tajiri zaidi ktk Asia

Anasema mafanikio ya SIA yalichagizwa pia na uamuzi wa kujenga uwanja wa ndege wa Changi kuanzia 1978 mpaka 1984 walitumia  S $ 1.5 bil. Ukiwa ni uwanja mzuri kuliko yote ktk Asia

FIGHTING TRAFFIC CONGESTION
Anasema tatizo la foleni ktk peak hours lilikuwa kubwa sana 1975, alisoma ktk gazeti moja kuwa ili kupunguza foleni, basi magari yanoingia katikati ya mji yalipie na yawe na stika. Basi wakapanga kuwa magari yatayobeba abiria wanne yapite bila stika vinginevyo mengine yalipie S$ 3 kila siku na ilipwe kwa mwezi. Anasema hata hivyo watu walilipia na foleni ikarudi baada ya muda mfupi

Baadae wakaja na mpango kuwa kama mtu anataka kununua gari inabidi kwanza aombe kibali ambapo atakubaliwa namba ya vibali kwa mwaka haijazidi uwezo wa barabara. Vilevile wakaongeza ushuru na kodi kwa kuingiza magari , hii iilsaidi kiasi, baadae walianzisha underground BRT, na kupunguza tatizo la foleni

DELICATE MALAY ISSUES
Jamii ya wamalay walikuwa wakiishi pamoja katika makazi dini, ila baada ya serikali kuanzisha mpango wa nyumba kwa kila familia waliweza kupata makazi bora
Pai watoto wao walikuwa wakifanya vibaya shuleni katika hesabu kwa kushirikiana na wabunge waliweza ku adress hiyo issue na kuwawekea mpango maalum wa tuishen na kuwaelemisha wazazi wawafuatilie watoto nyumbani ktk homeworks na hatimaye tatizo hilo lilikwisha.

A STEP TOWARDS IT
Anaongelea kuhusu matumzi ya technolojia ya habari na mawasiliano, ambapo mpaka sasa ktk Singapore kila mwanafunzi wa sekondari ana komputa, anaelezea pia jimsi alivyopata shida kuanza kujifunza komputa lakini baadae alizoea

A CHIEF JUSTICE, A PRESIDENT
Anaelezea alivyokuwa akifanya baadhi ya teuzi kwa kuwashirikisha wadau, mfano kuna wakati alitakiwa kumteua jaji mkuu, basi aliwaita majaji kila mtu kwa muda wake na kumwambia kama angekuwa anamteua  jaji mkuu angemteua nani, basi wakaandika majina na jina lililopata kupendekezwa zaidi ndo akamteua jaji mkuu, uteuzi ambao ulifurahiwa na wengi.

CHAPTER 16:

UPS AND DOWNS WITH MALAYSIA

Mwandishi anaanza kwa kueleza kuwa miezi 8 baada ya kutengana na Malaysia tarehe 20/3/1966, waziri mkuu wa Malaysia Tunku Abdul Rahman alitembelea Singapore ambapo alimshutumu mwandishi kwa kutoruhusu wahamiaji kutoka Malaysia wanaotafuta kazi Singapore na pia kumlaumu kuwa mawaziri wake Chin Chye na Raja walikuwa wakiikashfu Malaysia katika hotuba zao,
Mwandishi anasema kuwa alimjibu kuwa halikuwa jukumu la Singapore kuwapa ajira raia wa Malaysia na kuhusu mawaziri alijibu kuwa labda bado walikuwa hawajazoea kuwa wametengana na Malaysia na kuwa angewaambia waache kutoa matamshi ya aina hiyo
Anasema Tunku alikuwa na kiburi sababu mwandishi alifanya kazi chini yake ktk muungano na pia alikuwa na bataliani ya jeshi lake ktk Singapore vilevile walikuwa wakipata maji toka Malaysia.

Anasema kuwa jambo kubwa lililochangia kuvunjika kwa muungano baina yao ni Malaysia kuendekeza sera za uzawa (Malaysia for Malays) ampabo wazawa walipewa upendelea zaidi ya watu wa asili nyingine, wakati wabia wao yaani Singapore walitaka Haki sawa kwa wote(Malaysia for Malaysians)

Mwandishi anasema Tunku alitaka hata kuwachagulia Singapore washiriki , mfano baada ya Indonesia kuitambua Malaysia, mwezi April,1966, Malaysia walipiga mkwara kuwa Indonesia ingeweza kutumia ardhi ya Singapore kuishambulia Malaysia. Mwandishi anasema waliwajibu kuwa hawakuwa na haki ya kuwachagulia marafiki au maadui.Baada ya Indonesia kuitambua Singapore.

Wakati wa uchaguzi wa Malaysia  mwaka 1969 kulitolewa tuhuma kuwa Chama cha PAP kilikuwa kikisaidia  chama cha DAP cha Malaysia, mwandishi anasema walimwandika Tunku kuhusu madai hayo ambapo alisema ni kweli wanaingilia mambo ya Malaysia.
Uchaguzi ukipofanyika chama cha Tunku(UMNO) kilupoteza viti 8, baadae Mei 1969 kulitokea machafuko ya kikabila ambapo watu 800 waliuwawa,. Kesho yake mfalme akatangaza hali ya hatari na kumteua Razak k6wa mwenyekiti wa kamati ya usalama, umaarufu wa Tunku ukazidi kushuka hadi tarehe 31/8/1970 alipotoka madarakani

Baada ya Tunku kutoka madarakani aliingia Razak kama waziri mkuu, anasema Razak aliendeleza sera za uzawa na hakuwa na mahusiano mazuri na Singapore, anasema mahusiano yalirejea kuwa kazuri miaka ya 1980 wakati waziri mkuu wa Malaysia akiwa  Hussein Onn ambaye alichukua ofisi Januari 1976 baada ya Razak kufariki kwa kansa ya damu. Anasema Hussein hakiwa mbaya ila aliathiriwa na maamuzi ya chama chake cha UMNO, Hussein alijiuzuru mwaka 1981, na akaingia Dr. Mahathir Mohamad, huyu alikuwa mwelewa zaidi ja hakukumbatia sera za uzawa, alikuwa tayari kujifunza na kujirekebisha. Anasema chini yaMahathir Singapore na Malaysia zilirejesha mahusiano yenye faida kwa pande zote.
FROM THIRD WORLD TO FIRST. FROM THIRD WORLD TO FIRST. Reviewed by Maktaba on May 17, 2017 Rating: 5

2 comments:

  1. Uchambuzi murua sana, kongole sana mchambuzi wetu ndugu Kamugisha S.

    ReplyDelete
  2. uchambuzi mzuri sanaaaaaaa!!!

    ReplyDelete

Powered by Blogger.